0
Per Mertesacker akionyeshwa kadi nyekundu.
Costa akiwa amelala baada ya kuangushwa.
Per Martesacker akitoka nje
Wenger akilalamika
LONDON, ENGLAND

BOSI wa Arsenal, Arsene Wenger amesema timu yake kwa mara nyingine imekuwa mhanga wa straika wa Chelsea, Diego Costa baada ya beki wake, Per Mertesacker kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye kipigo cha Jumapili.
Mertesacker alitolewa nje katika dakika ya 18 baada ya kumkwatua Costa ambaye ndiye aliyefunga bao la ushindi la Chelsea.


Giroud akiwa nje"Costa amewafanya wachezaji wetu wawili kutolewa nje katika michezo miwili dhidi ya Chelsea," alisema Wenger.
"Uamuzi huo ni sawa au si sawa? Sifahamu. Huo ndio ukweli, bila ya kumshtumu kwa lolote."
Costa pia alihusika katika ugomvi uliomfanya beki wa Arsenal, Gabriel kutolewa nje katika mchezo wa Septemba ambao Chelsea ilishinda mabao 2-0.
Kadi hiyo ya Mertesacker ilibadilisha mchezo katika Uwanja wa Emirates na kuifanya Arsenal kupokea kipigo kuifanya kuwa nyuma kwa pointi tatu mbele ya vinara wa ligi hiyo Leicester.
Ni kadi ya saba kwa Arsenal kuonyeshwa dhidi ya Chelsea – ni nyingi kuliko za timu nyingine – na ni ya tatu katika msimu huu dhidi ya Chelsea ukijumlisha na ile ya Santi Cazorla pale Stamford Bridge.
Costa alifungiwa michezo mitatu baada ya mchezo kutokanana kugombana na Laurent Koscielny.
Wenger aliongeza : "Sijui kama Costa alikuwa amezidi au hapana au kama Per Mertesacker alimgusa au hapana. Ni uamuzi ambao tunapaswa tuukubali nadhani tumefanya hivyo.
"Mwamuzi alikuwa na haraka sana wa kutoa kadi nyekundu. Tumekubaliana na uamuzi na ilipaswa tupate hata sare. Tulikuwa na nafasi. Kiakili tulikuwa makini. Kuna wakati unaweza ukapoteza mechi na ukawapongeza wachezaji wako."
Alipoulizwa kama anadhani Costa ametengeneza mazingira ya kadi hiyo nyekundu, Wenger alisema: "Ndio. Huo ndio mchezo wa straika. Diego Costa ni mzuri katika hilo."
Baada ya kadi nyekundu ya Mertesacker, Wenger alimtoa mfungaji bora wa klabu hiyo Olivier Giroud na kumwingiza beki Gabriel.
Kwa hiyo mbele akawacha Theo Walcott na Joel Campbell wakiwa ni washambuliaji tegemeo, wote wawili aliwatoa  na nafasi zao zikachukuliwa na Alexis Sanchez na Alex Oxlade-Chamberlain.

Giroud na Martesacker wakiwa katika suti.Wenger alisema: " Unataka kucheza bahati nasibu katika kufanya uamuzi? Nadhani ulikuwa ni uamuzi mzuri.
"Tulitakiwa kushambulia na kuzuia nafasi. Ni kweli kwamba tulihitaji nguvu ya kushambulia kwa kushtukizana tuhilihaji kukabiliana –ndio maana kwanini nilifanya uamuzi huo."
Hiki ni kipigo cha tano cha Arsenal katika msimu cha kwanza katika uwanja wake wa nyumbani tangu ilipofungwa na West Ham mabao 2-0 katika mchezo wa ufunguzi.
Mchezo huo umeiacha Arsenal katika nafasi ya tatu pamoja na kulingana pointi na Manchester City  na kutofautiana kwa mabao ya kufunga na mabingwa hao wa msimu wa 2013-14 wa Ligi Kuu na ina tofauti mbili na wapinzani wao wakubwa wa London ya Kaskazini, Tottenham inayoshika nafasi nne. Ushindi huo umeifanya Chelsea kupanda hadi nafasi ya 13.

 

Post a Comment

 
Top