0
                           PARIS, UFARANSA
SIKU zote mwenye pesa ndiye anayekula vitu vizuri. Matajiri wa Paris, PSG wanataka kuteka soka la Ulaya kwa sasa ambapo, wanajiandaa kunasa huduma ya kiungo fundi wa Chelsea, N'golo Kante.
Tayari kwenye kikosi chao kuna, Neymar, Kylian Mbappe, Edinson Cavani na sasa wanamtaka staa wa Arsenal, Alexis Sanchez na Kante ili kuwaunganisha pamoja klabuni hapo.
Kante amekuwa mmoja wa viungo bora kabisa duniani kwa sasa, ambapo amesaidia klabuni yake ya zamani, Leicester City kubeba taji la England kwa mara ya kwanza kisha akatua Chelsea na kufanya hivyo msimu uliopita.
Matajiri wa PSG wametenga dau la Pauni 90 milioni kwa ajili ya kumnasa Kante kwenye dirisha la usajili la majira ya kiangazi.
Katika sirisha lililopita PSG walilipa Pauni 198 milioni kumsajili Neymar kutoka Barcelona kisha ikamchukua Mbappe kwa mkopo kwa makubaliano ya kulipa Pauni 168 mwishoni mwa msimu huku tayari ikiwa na mastaa kibao kikosini.
Kocha Unai Emery anataka kujenga kikosi cha kibabe mbacho kitakuwa tishio barani Ulaya na kubeba mataji kwa kadiri wanavyotaka.

Hata hivyo, Emery atakuwa na kibarua kigumu kupata saini ya Kante, ambaye kwa sasa anatajwa kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Muitaliano Antonio Conte.
Chelsea ilimnunua Kante kwa Pauni 32 milioni, baada ya kuizidi kete Manchester United iliyoingia vitani kuwania saini kiungo huyo.

Post a Comment

 
Top