MANCHESTER,
ENGLAND
ERIC
BAILLY wa Manchester United, ataukosa mchezo wa fainali wa Europa League baada
ya kutolewa nje kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Celta Vigo, John Guidetti
katika mchezo wa nusu fainali Alhamisi usiku uwanjani Old Trafford.
Beki
huyo wa kati alihusishwa katika vurugu zilizotokea katika dakika za mwisho
baada ya kunyoosha mkono usoni kwa mshambuliaji wa Certa –Vigo, John Guidetti
kabla ya kufichuliwa na mfungaji wa Celta, bao la kusawazisha la beki wa Certa-Vigo,
Facundo Roncaglia.
Mwamuzi
kutoka Romania, Ovidiu Hategan aliona beki huyo wa kimataifa wa Ivory Coasta
alistahili kadi nyekundu ya moja kwa moja – ikimaanisha Bailly atakosa fainali
itakayopigwa dhidi ya Ajax jijini Stockholm atakapokuwa akiutumikia adhabu yake.
Bailly akitoka uwanjani.Pia, Roncaglia naye alionyeshwa kadi nyekundu katika tukio hilo ambalo lilishudia Bailly na mchezaji mwenzake wa Man United Antonio Valencia wakipambana na Roncaglia katika ugomvi mkubwa uliolihusisha kundi kubwa la wachezaji wa timu hizo.
Kocha
wa United, Jose Mourinho alisema: “Sijaliona tukio hilo lakini yeye (Bailly)alikuwa
amependwa na mzuka kwa kuwa mchezo ulikuwa na hisia hadi mwisho wake kwan kila
mmoja. Baadhi e walistahamili kuliko wengine.
Mourine Fellaini akijaribu kumtuliza Bailly
“Nadhani
alikuwa na Roncaglia; Roncaglia siyo mgeni katika matukio kama haya na nadhani
bila ya shaka ni mtukutu.
“Tumempoteza
mchezaji muhimu sana katika fainali.”
United
itacheza na Ajax jijini Stockholm, Sweden Mei 24 na imekuwa na imekumbwa na matatizo katika nafasi ya beki
wa kati msimu huu.
Bailly
alipangwa sambamba na Daley Blind Alhamisi usiku lakini Chris Smalling ndio
kwanza amerudi kutoka katika majeraha ya goti. Phil Jones amepata nafuu na
kuanza alikaa benchi dhidi ya Celta baada ya kupona majeraha yake ya mguu.
Mwamuzi Avidiu akitimiza majukumu yake.
Bao
la Marouane Fellaini liliipeleka United katika fainali ya Stockholm, pamoja na
kwamba Roncaglia alisawazisha na kuwafanya vijana wa Mourinho kushinda mabao
2-1 katika matokeo ya jumla.
Post a Comment