0


MANCHESTER, ENGLAND
BASTIAN SHWEINSTEIGER (pichani) baada ya kuchaguliwa kuwamo kwenye kikosi cha Ligi Kuu, sasa ameondolewa kwenye kikosi cha Manchester United kitakachoshiriki  Europa League.
Schweinsteiger, 32, ni mchezaji pekee aliyeyoko kwenye kikosi hicho cha Ligi Kuu ambaye hajaorodheshwa kwenye kikosi kitakachoshiriki michuano hiyo ya Ulaya.
Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani hajacheza hata dakika moja katika klabu hiyo tangu Kocha Jose Mourinho aanze kazi na ameamua kubaki Old Trafford kuliko kuondoka kwenye dirisha la usajili lilifungwa Septemba Mosi.

"Bila shaka, ndoto yangu ni kuitumikia Manchester United na kuisadia kutimiza malengo iliyojiwekea," Schweinsteiger alisema mapema wiki hii.
"Tulifanya mazungumzo na sina tatizo na Jose Mourinho. Tuna mawasiliano mazuri na ameniambia mambo ya upande wake na pia najua ninachokitaka. 
"Tunapaswa kusubiri na kuona mambo yatakayotokea Septemba na Oktoba, lakini kuna heshima kati yetu na hilo ni jambo muhimu kwangu. Nina uhakika sitaacha kucheza soka.”
Schweinsteiger anakosa nafasi katika Europa League kwa sababu nafasi 2 1 zinapatikana kwa wacheza ambao hawajakuzwa na klabu. Man United ina wachezaji 22 akiwamo mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani.
United ina nafasi ya kuingiza wachezaji wawili tu katika kikosi hicho ambao wamekuzwa na klabu na ambao waliokuwapo kwenye kikosi hicho kwa miaka mitatu wakiwa na umri wa miaka kati ya 15 na 21.
Wachezaji Wayne Rooney na Jesse Lingard wanaangukia katika kipengele hicho, kitu kinachomaanisha United inaweza kutaja kikosi cha wachezaji 23.
Wachezaji wa kikosi cha kwanza Timothy Fosu-Mensah, Marcus Rashford na Luke Shaw wamefuzu kutokea kikosi cha B – kwa wachezaji waliozaliwa baada ya  mwaka 1994 ambao wameendelea kusajiliwa kwa miaka miwili mfululizo.

United imepangwa na katika Kundi A sambamba na Fenerbahce, Feyenoord na Zorya Luhansk. Itaanza kampeni yake uwanjani  Feyenoord Septemba. 15.
Kikosi kamili ni kama ifuatavyo: Bailly, Blind, Carrick, Darmian, De Gea, Depay, Fellaini na Herrera.
Wengine ni Ibrahimovic, Johnstone, Jones, Lingard, Martial, Mata, Mkhitaryan, Pogba, Rojo, Romero, Rooney, Schneiderlin, Smalling, Valencia na Young.

Post a Comment

 
Top