MANCHESTER,
ENGLAND
PEP
GUARDIOLA ametupiwa lawama kutokana na kumdhalilisha kiungo, Yaya Toure (pichani juu) kwa
kumuacha nje ya kikosi cha Manchester City kitakachocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya
hatua ya makundi, kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo.
Kiungo huyo
wa Ivory Coast mwenye umr wa maika 33-aliachwa katika hatua hiyo Ijumaa
iliyopita bila ya kupewa taarifa na Kocha, Guardiola.
Guardiola
Hata hivyo, Yaya
hajakitumikia kikosi cha City katika Ligi Kuu baada ya michezo mitatu chini ya
kocha huyo mpya.
Na pigo
lingine, kiungo huyo wa zamani wa Barcelona ambaye amebakisha msimu mmoja
katika mkataba wake na City - sasa anapaswa kukubali kutokuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza
katika Kundi C dhidi ya Barcelona, Borussia Monchengladbach na Celtic
ambayo anaichezea kaka wa Toure, Kolo.
Wakala wa Toure,
Dimitri Seluk, amelalamika kwamba shinikizo kubwa sasa ni Guardiola kushinda lakini
alisisitiza mteja wake atauangalia msimu wote huu akiwa nje ya Uwanja wa Etihad.
Seluk alisema: “Ni
uamuzi wa Pep na tunapaswa kuheshimu hilo.
...Yaya akipambana
“Kama atashinda Ligi
ya Mabingwa akiwa na City msimu huu nitasafiri hadi England na nitazungumza
kwenye runinga kwamba Pep Guardiola ni kocha bora duniani.
“Lakini kama City haitashinda
Ligi ya Mabingwa ninatarajia kwamba Pep atakuwa na jukumu la kumuomba msamaha
Yaya Toure kwa kusema kwamba alikosea kumdhalilisha mchezaji mkubwa kama Yaya.
“ Lakini ninachotaka
kuwambia ni kwamba Yaya atamaliza msimu wake akiwa na City. Hataondoka katika
dirisha la usajili la Januari. Anatarajia kwamba atapata nafasi ya kuonyesha uwezo
wake.”
Toure na kipa mpya wa Man City,
Claudio Bravo aliyenunuliwa kwa dau la Pauni 17 milioni kutoka Barcelona ndio
wachezaji pekee katika kikosi cha City ambao wameonja utamu wa kubeba taji la
ubingwa wa Ulaya.
Toure
alikuwa katika kikosi cha Barcelona kilichoichapa Manchester United 2-0 jijini
Rome mwaka 2009.
Hata
hivyo, mwaka 2010 Guardiola alimuuza Toure kwa dau la Pauni 24 milioni kwenda
Manchester City na ujio wake City ulitabiriwa ungehitimisha maisha ya soka ya
staa huyo.
Toure
alikataa ofa za kutoka klabu mbalimbali za China ambazo zingemuongeza mshahara
mkubwa kuliko ule anaolipwa na City kwa sasa, lakini pia alikuwa anahusishwa
kuungana na kocha wake wa zamani wa City, Roberto Mancini katika kikosi cha
Inter Milan.
Hata
hivyo, baada ya mazungumzo ya kina na Guardiola kocha huyo alimuomba abaki
kikosini hapo kwa miezi 12 iliyobaki ili amsaidie kuzoea mazingira ya klabu
hiyo pamoja na soka la England kwa ujumla, lakini sasa amemuacha katika kikosi
cha Ulaya.
Yaya akiwa na Guardiola Barcelona
Inaeleweka
kuwa Guardiola na benchi lake la ufundi walikuwa wanaumiza kichwa mchezaji wa
kumuacha katika orodha hiyo kati ya Toure na beki wa kimataifa wa kimataifa wa
Ubelgiji, Vincent Kompany, ambaye alikuwa majeruhi wa muda mrefu.
Hata
hivyo, Kompany amefanikiwa kucheza mechi moja ya kirafiki kwa ajili ya kupima
afya yake na anaweza kurejea uwanjani muda wowote kuanzia sasa, kitu ambacho kimemfanya
Guardiola alikate jina rasmi la Toure katika orodha ya wachezaji 21
waliopelekwa Uefa.
Orodha
kamili ya kikosi cha City ambacho imepelekwa Uefa ni Claudio Bravo, Willy
Caballero; Bacary Sagna, Vincent Kompany, Pablo Zabaleta, Aleksandar Kolarov,
Gael Clichy, John Stones, Nicolas Otamendi; Fernando, Raheem Sterling, Ilkay
Gundogan, Jesus Navas, Kevin De Bruyne, Fabian Delph, Leroy Sane, David Silva,
Fernandinho; Nolito, Sergio Aguero, Kelechi Iheanacho.
Post a Comment