0


LIVERPOOL, ENGLAND
KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesisitiza kwamba ana kauli ya mwisho katika kufanya usajli mpya ndani ya Anfield.
Mtangulizi wake, Brendan Rodgers ambaye alifukuzwa kazi Oktoba, ameiambia Sky Goals Jumapili iliyopita kwamba maamuzi mengi ya usajili yalikuwa yakiamuliwa na kamati ya usajili.
Kwa upande wake, Klopp alisema ana kura ya  kufanya uamjuzi juu ya mazungumzo ya kufanya uhamisho wa mchezaji katika klabu.

“Kama kwa mfano nikisema ninamtaka Zlatan Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35, na tunatakiwa kumlipa Pauni 100 milioni  labda hapo ninaweza kuwauliza mabosi kabla sijaingia naye makubaliano.
'Lakini  ni kama nilivyosema siku ya kwanza niliyokuja hapa; Ni kama  nilivyozea kufanya kazi. Kuna wakati mimi na wenzangu tunaweza kuwa na mawazo kuhusu mchezaji tunayemjua au tuliyesikia habari zake na tunakusanya baadhi ya taarifa kuhusu hilo.
‘Kama simtaki mchezaji kuja hapa, hatakuja na kama mchezaji ninayemtaka hajakidhi bajeti yetu hawezi kuja pia. Hiyo ni kawaida.”
Rodgers alionekana kwa mara ya kwanza kwenye runinga tangu alipoondoka Liverpool na kuweka wazi kwamba hakuwa na nguvu ya kuamua kusajili wachezaji.
'Ulikuwa ni uamuzi wa kikundi, kweli,' Rodgers alisema. ‘Hakikuwa kitu ambacho ningekuwa na uhakika wa kukitolea uamuzi wa mwisho,” aliongeza Rodgers. 
“ Kama kocha unakuwa ni nembo ya klabu lakini kulikuwa na timu ya kusajili. Watu ambao walikuwa wakifanya kazi kubwa ya klabu.”
Liverpool itakuwa uwanjani Anfield Jumatano, itakapocheza na Exeter katika mchezo wa marudiano wa  Kombe la FA.  Katika mchezo uliopita timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.



Post a Comment

 
Top