LONDON, ENGLAND
JOHN TERRY hatakuwamo kwenye ufalme wa
bosi mpya wa Chelsea, Antonio Conte wakati Juan Cuadrado anaweza kurudishwa
kundini ili kupewa nafasi ya kutengeneza kikosi kipya cha Chelsea.
Kocha Conte pia anatarajiwa kufanya
mazungumzo na mchezaji asiyekuwa na furaha ndani ya kikosi hicho, Diego Costa ili
aendelee kubaki.Wakati nahodha Terry akionyeshwa mlango wa kutokea, bosi Conte ataachana na kipa wa kikosi hicho, Thibaut Courtois na nafasi yake itazibwa na kipa wa Southampton, Fraser Forster.
Chelsea inataka kubaki na Eden Hazard, lakini hofu iliyopo ni kwamba kichwa chake kimetawaliwa na fikra za kujiunga na Paris Saint-Germain.
Bosi huyo wa Italia pia anataka kumrudisha winga, Cuadrado na kumpa nafasi ya kuweza kufufua matumaini yake ya kubaki Chelsea kufuatia kutolewa kwa mkopo Juventus ya Italia.
Habari zinasema, Costa atahitimisha listi ya Conte baada ya kufanya mazungumzo na kocha huyo kabla ya kuanza kazi pindi Italia itakapotolewa katika mashindano ya Euro 2016.
Marafiki wa Costa ambao ni wachezaji wenzake wa Chelsea wanaamini kwamba straika huyo wa kimataifa wa Hispania ameshaitengeneza akili yake katika kutaka kuondoka England baada ya misimu miwili mchanganyiko tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Atletico Madrid, ambayo inataka kumrudisha kundini.
Conte, ni shabiki wa straika huyo mwenye rekodi ya kuvutia ya kufunga mabao 35 katika michezo 74 lakini pia amekuwa akihusika katika mabishano na kulalamikiwa na ametolewa mara moja kwa kadi nyekundu.
Costa
Conte, mchezaji wa zamani wa
kimataifa wa Italia ambaye aliwahi kuichezea na kuifundisha Juventus atakabidhiwa
pesa za usajili wa kuiingiza Chelsea katika changamoto na kuirudishia heshima baada
ya kuwa na msimu mbaya.Kocha wa Leicester ambaye zamani aliwahi kuinoa Chelsea, Claudio Ranieri, alikuwa bosi wa kwanza kufukuzwa na tajiri wa Chelsea, Roman Abramovich, alisema: “Conte atafanya vizuri. Lakini itakuwa vigumu kidogo tofauti na inavyotarajiwa. Ninaamini atataka kufanya kila kitu mwenyewe. Chelsea haitaweza kumruhusu kufanya hivyo.”
Kocha Conte anataka kufanya usajili wachezaji watano-mabeki wa kati wawili, viungo wawili na straika mmoja hata kama Costa atabaki.
Monalas
Beki wa Roma, Mgiriki, Kostas
Manolas ni chaguo la kocha Conte katika safu ya ulinzi wakati Chelsea pia inataka
kumrudisha beki Mdenmark, Andreas Christensen ambaye yupo kwenye mkopo Borussia
Monchengladbach wa mwaka mmoja.Wachezaji wa Roma, Radja Nainggolan na Miralem Pjanic pamoja na yule wa Bayern Munich, Arturo Vidal ni kati ya viungo ambao Conte anawatolea macho.
Vidal
Katika safu ya ushambuliaji, straika
wa zamani wa Chelsea Romelu Lukaku, ambaye Everton inamtaka kwa Pauni 60 milion,
na Ganzalo Higuan wa Napoli wanatazamwa na Conte kwa jicho la karibu.Kwa kulipata dili hili, Conte amefanikiwa kuziba nafasi ya aliyekuwa kocha wa kudumu, Jose Mourinho baada ya kufikia makubaliano ya idadi ya maofisa ambao watakuwa wakimsaidia kazi yake.
Hazard
Kocha Conte aliwataka watu 10 ambao
alikuwa akifanya nao kazi katika timu ya taifa ya Italia lakini maafikiano ya
pande mbili yamekubaliana watu watano tu.Kaka wa Conte, Gianluca atawasili kama kocha msaidizi sambamba na Angelo Alessio, Massimo Carrera, Paolo Bertelli na Mauro Sandreani wote watakuwa na majukumu katika kikosi hicho.
Higuan
Chelsea imemtaka Conte kuwatafutia
nafasi kocha msaidizi wa sasa, Steve Holland, kocha wa viungo, Chris Jones na
kocha wa makipa, Christophe Lolichon.
Lukaku
Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa
wa Italia amepewa mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Pauni15 milioni na
pia atavuna bonasi ya Pauni 5 milioni kama atashinda taji la Ligi ya Mabingwa.
Post a Comment