0


                     MADRID, HISPANIA
CRISTIANO RONALDO ameonyesha hisia na kuguswa na kifo cha baba yake.
Baba huyo, José Dinis Aveiro alifariki dunia wakati supastaa huyo wa Real Madrid akiwa na umri wa miaka 20 kutokana na kufeli kwa ini.
Awali, Ronaldo alikiri kutokuwa na uhusiano mzuri na baba ambaye alikuwa muathirika wa ulevi.
Lakini staa huyo wa kimataifa wa Ureno alionyesha kuguswa na kifo hicho kwa kuweka picha ya baba yake nyuma akiwa na wanawe Cristiano Jr na pacha wake.
Picha hiyo ya familia ilipigwa mbele ya picha ya kuchorwa ya Aveiro.
"Siku zote utakuwa nasi," Ronaldo alindika.
Aveiro alifariki dunia Septemba 2005 wakati huo Ronaldo akiwa anaichezea Manchester United.
Staa huyo mwenye umri wa miaka 32 alimpongeza kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kwa kushiriki kwenye msiba huo.
Ronaldo alizungumza kwa uwazi  kuhusu baba yake mwaka 2015, akikiri: "Sikuweza kumfahamu kwa kweli, kutoka moyoni na sikujua kwa nini alikuwa akinywa pombe, labda alichanganyikiwa na maisha yake.
"Nilihitaji baba mwingine, ambaye angekuwapo sasa kuona mafanikio yangu."

Ronaldo aliendeleza wakati wake mzuri baada ya katikati ya wiki kuisaidia Real Madrid kuifunga Borussia Dortmund.
Supastaa huyo alifunga mara mbili na anatarajiwa kuongeza rekodi yake ya ufungaji dhidi ya Espanyol Jumapili.

Post a Comment

 
Top