QUITO,
ECUADOR
KUNA
Lionel Messi mmoja tu duniani. Huyu hapa wa Jumatano usiku pale Ecuador.
Amefanya maajabu ambayo dunia ilikuwa inamtarajia ayafanye na kweli akayafanya.
Amepiga ‘hat trick’ ambayo imeipeleka Argentina katika fainali za Kombe la Dunia
mwakani.
Argentina
ilikuwa inakaribia kuzikosa fainali hizo na ilihitaji kushinda mchezo huo wa
ugenini Ecuador katika Jiji la Quito ambalo lipo futi 9350 kutoka usawa wa
habari huku kukiwa na hali ya hewa nzito. Messi akasahau yote hayo na kuibuka
shujaa wa Wargentina.
Ushindi
huo wa mabao 3-1 sasa umeipeleka Argentina mpaka nafasi ya tatu katika kundi
lao la Amerika Kusini na kuungana na Brazil, Uruguay na Colombia kufuzu moja
kwa moja katika fainali hizo zitakazofanyika Russia Juni mwakani huku Peru ikisubiri
kucheza pambano la mtoano na New Zealand.
Hata
hivyo, mambo yalianza kuwa mabaya kwa Argentina katika sekunde 40 tu za pambano
hilo baada ya kutanguliwa kwa bao la Ecuador lililofungwa na Renato Ibarra.
Kuanzia hapo Messi alionyesha kiwango bora zaidi kwa mchezaji binafsi katika
jezi ya Argentina.
Alifunga
bao la kusawazisha katika dakika 12 kabla hajaongeza jingine dakika nane
baadaye katika dakika ya 20. Kipindi cha pili, Messi aliufunga mchezo kwa
kupiga hat trick katika dakika ya 62 na hivyo kuinyamazisha dunia ambayo
ilikuwa na wasiwasi huenda Argentina isifuzu Kombe la Dunia.
Hiyo
ilikuwa hat trick yake ya 44 katika maisha yake ya soka na pia amerudisha
uwezekano wa kutwaa taji la Kombe la Dunia, kitu ambacho amekuwa akikisubiri
kwa hamu katika maisha yake yote ya soka tangu awe staa.
Kocha
wa Argentina, Jorge Sampaoli mara baada ya pambano hilo alidai Messi ndiye
mchezaji bora zaidi duniani kwa sasa huku Messi alikuwa hadaiwi Kombe la Dunia
na Argentina, bali Kombe la Dunia lilikuwa linamdai Messi.
“Leo
kwa bahati tu utaifa wa mchezaji bora zaidi duniani ni wa Muargentina. Lazima
tuhakikishe sio kila kitu kinamtegemea Messi lakini leo ameonyesha uwezo wake.
Niliwaambia wachezaji, ‘Messi alikuwa hadaiwi Kombe la Dunia na Argentina, bali
Kombe la Dunia lilikuwa linamdai Messi’ Tumsaidie afike katika Kombe la Dunia,”
alisema Sampaoli.
“Nadhani
mechi ilianza kutuchanganya kwa maana ya mipango yetu ilikuwa migumu zaidi kwa
sababu Ecuador ilifunga bao katika dakika ya kwanza. Hata hivyo, sisi kama
kundi tuliamini mechi inaisha katika dakika 90,” alisema Sampaoli.
Na
sasa Messi anakwenda katika fainali za Kombe la Dunia sambamba na staa mwenzake
katika soka la kileo, Cristiano Ronaldo ambaye aliiongoza Ureno kuichapa Uswisi
katika mchezo muhimu wa Ureno na hivyo kujihakikishia safari ya Russia. Hata
hivyo, Ureno haikuwa katika tishio kubwa kama Argentina.
Mastaa
wakubwa ambao wataikosa safari ya Russia ni pamoja na nyota wawili wa Chile,
Alexis Sanchez na Arturo Vidal ambao katika mchezo wa mwisho dhidi ya Brazil
juzi usiku walichapwa mabao 3-0 na Brazil katika Jiji la Sao Paulo, Brazil.
Staa
mwingine ambaye atazikosa fainali hizo ni nyota wa kimataifa wa Wales, Gareth
Bale ambaye kikosi chake cha Wales licha ya kuonyesha mambo makubwa katika Euro
2016 iliyofanyika Ufaransa lakini kimeshindwa kuonyesha makali yake katika
mechi za kufuzu.
Mastaa
wengine wakubwa ambao watakuwepo katika fainali zijazo za Kombe la Dunia ni
pamoja na Neymar, Kylian Mbappe, Antoine Griezmann, Luis Suarez, Paul Pogba,
Eden Hazard, Alexandre Lacazette na wengineo.
2017 ford fusion hybrid titanium - TiG
ReplyDeleteDiscover titanium or ceramic flat iron premium and titanium exhaust premium titanium watches at a boutique boutique brand. Get grade 23 titanium the best 4x8 sheet metal prices near me deals titanium build and offers of TiG in an instant.