0


LONDON, ENGLAND
JOSE Mourinho hana kazi. Yuko nje ya kibarua lakini Mreno huyo ametumia pesa nyingi kuliko meneja mwingine yeyote ndani ya miaka 10.
Usajili wote alioufanya Mourinho (52) unafikia kiasi cha Pauni 619 milioni na anafuatiwa na  bosi wa Manchester City, Manuel Pellegrini  ambaye ametumia  Pauni 597 milioni na Carlo Ancelotti ,Pauni 466 milioni.

Kocha Pellegrini ametumia  Pauni 80 milioni kumnunua Cristiano Ronaldo wakati akiwa na Real Madrid mwaka 2009 na usajili wake mwingine ni ule aliowanunua Karim Benzema kwa Pauni 30 milioni na Xabi Alonso kwa Pauni 30 milioni.

Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal ameshika nafasi ya sita katika  kumi bora  baada ya kutumia Pauni 337 milioni.
Mourinho ameziongoza Real Madrid, Inter Milan  na Chelsea mara mbili ndani ya miaka 10 na ametumia Pauni 67 milioni msimu wa mwisho alipochukua ubingwa wa Ligi Kuu.

Hiyo ikijumuisha Pauni 30 milioni  kwa kumnunua, Cesc Fabregas kutoka Barcelona na Pauni 32 milioni kumnunua Diego Costa kutoka Atletico Madrid.
Pep Guardiola ataondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu anajipanga kwenda England, akiwa na umri wa miaka 44 anatarajiwa kujiunga na Manchester City.
Mhispania huyo ameiongoza Barcelona kwa miaka minne,ameshinda ligi  mara tatu na Ligi ya Mabingwa mara mbili, na amekuwa na Bayern  kwa miaka mitatu. Usajili wake umegharimu Pauni 382 milioni na kumfanya  kushika nafasi ya tano katika listi.

Bosi wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson naye yumo akiwa ameshika nafasi ya 10 akiwa ametumia Pauni 281 milioni kabla hajastaafu  mwaka 2013  katika miaka yake 26 akiwa na klabu hiyo.
Juu yake yupo kocha wa  zamani wa Liverpool, Brendan Rodgers ambaye ametumia Pauni 287 milioni na Kocha Arsene Wenger aliyetumia Pauni 333 milioni.
Arsenal iko kileleni katika Primia Ligi lakini Wenger anaweza kutumia pesa zaidi  katika usajili wa mwezi huu wa Januari ili kuweza kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu. Mara ya kwanza Wenger alichukua ubingwa huo mwaka 2004.

Wenger anaweza kumpita Van Gaal aliyetumia Pauni 337 milioni na kocha aliyefukuzwa wa  Real Madrid, Rafa Benitez aliyetumia Pauni 376 milioni kama ataamua kuimarisha kikosi chake.
TOP TEN
1 - Jose Mourinho – Pauni 619m
2 - Manuel Pellegrini –   Pauni 597m
3 - Carlo Ancelotti – Pauni 466m
4 - Roberto Mancini – Pauni 441m
5 - Pep Guardiola – Pauni 382m
6 - Rafa Benitez – Pauni 376m
7 - Louis van Gaal – Pauni 337m
8 - Arsene Wenger – Pauni 333m
9 - Brendan Rodgers – Pauni 287m
10 - Sir Alex Ferguson –Pauni 281 m.
PESA ILIVYOTUMIKA
Jose Mourinho 
Pauni 32m – Diego Costa
Pauni 30m – Andriy Shevchenko
Pauni 30m – Willian
Manuel Pellegrini
Pauni 80m – Cristiano Ronaldo
Pauni 54m – Kevin De Bruyne
Pauni 49m – Raheem Sterling
Carlo Ancelotti
Pauni 85m – Gareth Bale
Pauni 63m – James Rodriguez
Pauni 50m – Fernando Torres
Roberto Mancini
Pauni 40m – Sergio Aguero
Pauni 27m – Edin Dzeko
Pauni 25m – Samir Nasri
Pep Guardiola
Pauni 40m – Zlatan Ibrahimovic
Pauni 35m – Cesc Fabregas
Pauni 34.2m – David Villa
Rafa Benitez
Pauni 34.5m – Gonzalo Higuain
Pauni 22.6m – Danilo
Pauni 22.5m – Mateo Kovacic
Louis van Gaal
Pauni 59.7m – Angel di Maria
Pauni 36m, ikapanda hadi Pauni 57.6m – Anthony Martial
Pauni 31.5m – Luke Shaw
Arsene Wenger
Pauni 42.5m – Mesut Ozil
Pauni 35m – Alexis Sanchez
Pauni 16m – Santi Cazorla
Brendan Rodgers
Pauni 32.5m – Christian Benteke
Pauni 29m – Roberto Firmino
Pauni 25m – Adam Lallana
Sir Alex Ferguson
Pauni 30m – Dimitar Berbatov
Pauni 28m – Juan Veron
Pauni 27m – Rio Ferdinand



Post a Comment

 
Top