0


                NYON, SWITZERLAND
CRISTIANO RONALDO amekuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya mara tatu baada ya kunyakua tuzo ya msimu wa 2016-17 Alhamisi.
Staa huyo wa kimataifa wa Ureno aliwashinda nyota wa Barcelona, Lionel Messi na kipa wa Juventus Gianluigi Buffon katika tuzo hiyo ambayo ushiindi wake umechangiwa na klabu yake ya Real Madrid kutwaa mataji ya La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili.
Katika kura 80 za zilizopigwa na makocha wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League, waandishi wa habari 55, Wawakilishi wa kila chama mwanachama wa UEFA, Ronaldo alipata alama 482, Messi (141) na Buffon (109).
“Nina furaha sana kuwa hapa, na kutunikiwa ushindi huu kwa mara nyingine,” Ronaldo alisema. “Shukrani na hongera nyingi kwa wachezaji wenzangu. Nina furaha sana- shukrani pia ziende kwa mashabiki wa Real Madrid, na kwa kila mmoja aliyenisaidia kupata mafanikio.”
Ronaldo alimaliza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na mabao 42 katika michezo 46 aliyocheza, na kufuta misimu mibaya iliyokuwa ikimuandama tangu alipotua Bernabeu kutoka Manchester United mwaka 2009.
Ronaldo akiwa na tuzo yake.
Mabao12 ya Ronaldo yakiwemo mawili ya fainali na assisti nne katika michezo 13 ya Ligi ya Mabingwa iliwahakikishia vijana hao wa Zinedine Zidane kutengeneza historia ya kuwa timu ya kwanza kutetea taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika mfumo mpya. 

                                                        ...akiwa na Lieke Martens
  Katika hali ya kushangaza, Ronaldo pia alishinda tuzo ya Mshambuliaji Bora wa Ulaya pamoja na kwamba Messi ana jumla ya mabao 54 katika michezo 52 lakini amemshinda mpinzani wake huyo mkubwa na kutwaa Kiatu cha Dhahabu cha Ulaya.

Wachezaji wengine wa Real Madrid, Sergio Ramos na Luka Modric walijiunga na Ronaldo jukwaani baada ya kushinda Tuzo za Beki Bora wa Mwaka na Kiungo Bora wa Mwaka mtawalia.
Ronaldo na wawania tuzo wenzake
Buffon alitwaa Kipa Bora wa Mwaka wakati kiungo wa Uholanzi na Barcelona, Lieke Martens akitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwanamke wa Ulaya.

Post a Comment

 
Top