0


                     BARCELONA, HISPANIA
UNAWEZA isiiamini habari hii lakini huu ndio ukweli. Kuna uwezekano mkubwa kabisa  Barcelona FC ikahamia kucheza Ligi Kuu England. Hilo litawezekana tu kama mchakato wa kupiga kura kudai uhuru wa Catalunya utapitishwa Jumapili, waziri wa michezo amedai.
Hata hivyo, Serikali ya Hispania imepinga kwa kudai kuwa kura hiyo si halali na polisi imezuia masunduku ya kupigia kura. Waziri Mkuu wa Hispania Mariano amesisitiza kura hiyo kamwe haitakuwapo.
Kuna watu wengi wanaotaka uhuru wa Catalunya wanaokisiwa kufikia 7.5 milioni– kati yao akiwemo Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola – lakini vyama vyenye uaminifu kwa utawala wa Hispania vimekataa kupiga kura.
Kati ya mambo mengi yenye kuzua wasiwasi ni nini kitatokea iwapo Catalunya itakuwa nchi mpya kwa upande wa klabu za soka, ikiwemo Barcelona.
Waziri wa Michezo wa Catalunya Gerard Figueras alisema: “Katika suala la uhuru, timu za Catalunya zinazocheza Ligi ya La Liga – Barcelona, Espanyol na Girona – zitaamua wapi zinataka kucheza: katika Ligi ya Hispania au ligi za nchi jirani kama vile Italia, Ufaransa au Ligi Kuu England.
“Kwa sasa Hispania kuna timu kutoka nchi nyingine ambazo zinacheza ligi za taifa: Klabu kutoka Andorra katika soka na mpira wa kikapu. Monaco inacheza Ufaransa, katika England ni klabu kutoka Wales. Sidhani kama Uefa watakuwa na la kupinga kuona klabu nyingine zikicheza ligi nyingine kutoka nchi mwao.”

              Lionel Messi na Luis Suarez wataonekana England?
 Rais wa La Liga, Javier Tebas alisema: “Katika michezo, mambo lazima yawe wazi. Siyo rahisi kuwa na makubaliano na kuzisoma sheria za Hispania lakini kama klabu za Catalunya zitataka hivyo, hazitaweza kucheza La Liga, lakini naamini jambo kama hilo halitatokea."
Guardiola ambaye amesimama upande wa wawakilishi wa Catalunya, amesisitiza kuhusu uhuru.

                Wakatalinya wanataka kupiga kura Jumapili.
Akizungumza kwenye mkutano mwezi Juni, kocha huyo wa Manchester City alisema: “Hatuna uamuzi mwingine isipokuwa kupiga kura. Tunazitaka jamii za kimataifa ulimwenguni kote kutuunga mkono na juu ya demokrasia na kulinda haki ambayo inatishiwa Catalunya. Haki kama za kujieleza na kupiga kura.”

Wanafunzi wa Catalunya wakiandamana dhidi ya serikali ya Hispania.
Taarifa ya karibu kutoka Barcelona imesema: “FC Barcelona, inaheshimu uamuzi wa bodi ya wanachama, itaendelea kuunga mkono mahitaji ya watu wengi wa Catalunya na itafanya hivyo kwa njia ya amani na kwa kuonyesha mfano mzuri.”

Post a Comment

 
Top