MADRID,
HISPANIA
DIEGO COSTA atashuhudia mchezo wa timu zake mbili, Chelsea na Atletico Madrid uwanjani Wanda Metropolitano jijini Madrid, akiwa jukwaani.
DIEGO COSTA atashuhudia mchezo wa timu zake mbili, Chelsea na Atletico Madrid uwanjani Wanda Metropolitano jijini Madrid, akiwa jukwaani.
Pia, staa huyo
ataruhusiwa kutembea katika njia wanayopita wachezaji wanapotoka vyumbani na
kupata fursa ya kusalimina nao.
Kisha atapanda
jukwaani lakini habari kutoka Hispania zinasema hatarajiwi kuingia mbele ya uwanja
na kuonekana na mashabiki kama anavyotaka Kocha Simeone ili aweze kuzingatia
mechi hiyo.
Matukio hayo
yanakuja baada ya Jumanne usiku kukamilika rasmi kwa dili lake
la kurudi Atletico Madrid akitokea Chelsea baada ya pande timu hizo mbili
kukubaliana.
Dili la uhamisho la
Pauni 58 milioni litatolewa Januari huku staa huyo wa kimataifa wa Hipsania
akijaandaa kurudi tena mikononi mwa kocha wake, Diego Simeone.
Straika huyo mwenye
umri wa miaka 28- amesaini uhamisho wa mkopo hadi mwishoni mwa msimu, pamoja na
Atletico kuzuiwa kufanya uhamisho ikimaanisha hatacheza hadi Januari. Kisha
dili hilo litakuwa la kudumu hadi usajili wa majira ya joto.
Uhamisho wake utakuwa wa mkopo hadi Januari.
Atletico itamlipa Costa
mshahara wote wa Pauni 150,000 kuanzia sasa hadi majira ya joto ambapo
imekubalika kuwa ndio utafanyika uhamusho wa kudumu.
Nyota huyo wa
kimataifa wa Hispania atavaa jezi No18 akiwa katika mavazi ya Wanda
Metropolitano.
Diego Costa, amefunga
mabao 59 katika michezo 120 akiwa Chelsea – Ameshinda taji la Ligi Kuu mara
mbili na Kombe la Ligi, ana furaha kurejea katika Mji Mku wa Hispania.
Costa akishuhudia mchezo wa Atletico dhidi ya Sevilla.
“Nina furaha kurejea nyumbani, kila
siku nimekuwa nikisema hivyo, Atletico ni nyumbani, nina furaha, nimefurahi
sana,” alisema mara baada ya kujiunga na Altetico Madrid.
“Ningalia mbele
kuanza kutoa mchango wangu. Ninatarajia kujitoa kwa nguvu zangu zote kwa ajili
ya timu, kama siku zote nilivyokuwa nikijaribu kufanya.
“Juhudi maalumu zilizofanywa
na Miguel Angel Gil (Mkurugenzi Mkuu wa Atletico), na klabu nzima kwa jumla kwa
kukamilisha uhamisho huu, nina furaha na kila mmoja.”
Costa alimaliza
misimu mitatu akiwa mfungaji bora wa klabu wa kila msimu alipokuwa Stamford
Bridge baada ya kununuliwa kwa dili la Pauni 32 milioni akitokea Atletico Julai
2014.
Enzi zake akicheza dhidi ya Chelsea.
Hata hivyo, kukosana
kwake hadharani na Kocha wa Chelsea, Antonio Conte majira ya joto ilimaanisha
mwisho wake haukuwa mwema Magharibi mwa London.
Pia, mabingwa hao wa
Ligi Kuu England wamemtakia heri kufuatia kuondoka kwa Costa: “Tunamshukuru Diego
kwa jitihada zake na tunamtamka kila la heri.”
Post a Comment