0


                            LONDON, ENGLAND
ANTONIO CONTE (pichani chini) ameyadharau madai yaliyotolewa na straika wake, Diego Costa kufuatia mahojiano ya hivi karibuni akidai Chelsea inamtendea kama mhalifu.
Na kocha huyo wa Chelsea ameweka wazi msimamo wake kuwa straika huyo hakutakiwa kurudi katika mipango yake na kusisitiza mambo ya Costa yameshapita, pamoja na klabu kumtaka nyota huyo wa kimataifa wa Hispania kurudi Magharibi mwa London.
Conte alikumbana na swali hilo kwa mara ya kwanza tangu Costa alipofanya mahojiano, na kumtuhumu kocha huyo Muitaliano kumtendea kama mtuhumiwa na kudai hatarudi Chelsea hata kama klabu hiyo itendelea kumpiga faini.
Pia, Costa aliendeleza vita yake ya maneno na Chelsea na Conte kwa kudai mabingwa hao wa Ligi Kuu wanataka kumuuza bei ya ghali na kuzima ndoto zake za kurudi Atletico Madrid.
Chelsea inataka kumuuza Costa kwa Pauni 50 milioni, Atletico Madrid iko tayari kulipa Pauni 30 milioni.  Chelsea ilimnunua staa huyo kutoka Atletico Madrid mwaka 2014 kwa Pauni 32 milioni.

 “Ninachofahamu Chelsea inataka ofa kubwa kuliko ile iliyolipa kwa ajili yangu. Wakala wangu alisema Chelsea inataka pesa ambayo Atletico haitaweza kuikaribia. Lakini kama Atletico na Chelsea hazitafikia makubaliano na Atletico haitaonyesha jitihada, sitataka kuitumikia klabu ambayo haitaonyesha jitihada na kunisajili.
“Pindi niliposikia kuwa, Conte hanitaki, wakala wangu alizungumza na Atletico kama itataka nirudi.
“Bila shaka kwa moyo mkunjufu na heshima niliyoipata pale, walionyesha kuvutiwa. Lakini hawakulipa pesa. Atletico ni timu inayokua kila mwaka, ni timu kubwa lakini haiwezi kulipa kiasi kikubwa zaidi.

                    Costa akiwa nyumbani kwao, Brazil
"Chelsea ilipanga kuniuza katika klabu kadhaa, lakini nilikuwa muwazi kwao, Nilisema kama sipo katika mipango ya kocha, ninataka kuchagua sehemu ya kwenda. Sitawaachia wao waamue kwa kutaka pesa nyingi.’  
Alipoulizwa alichokisema Costa, Conte alicheka kabla ya kujibu: “Ni vizuri, ninapenda kucheka.
“Ninaweza kuwaambia kila mmoja aliyekuwa ndani ya Chelsea anafahamu nini kilitokea msimu uliopita kwa Diego. Sipendi kuendeleza hii kitu. Kwangu, imeshapita.”
Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA) kinaweza kutoa suluhisho la dharula kutokana na kuongezeka kwa mgogoro huu.

Kwa mtazamo wa Costa utahitajika usuluhishi wa PFA lakini chama hicho huwa kinawasaidia wachezaji ambao wako ndani ya klabu.
PFA iliwahi kuhusika kutatua mgogoro wa Luis Suarez na Liverpool miaka mitatu iliyopita wakati alipokatazwa kufanya mazungumzo na Arsenal.

Post a Comment

 
Top