0


                      LONDON, ENGLAND
DIEGO COSTA yuko umbali wa maili 5,000 kutoka Stamford Bridge akiwa mbali  zaidi kuunga na Kocha wa Chelsea, Antonio Conte.
Lakini Ijumaa straika huyo alitinga jezi ya Chelsea alipoenda kufanya mazoezi yake binafsi.
Costa kwa sasa anafanya mazoezi ya peke yake akiwa katika mji wa asili yake wa Lagarto baada ya kukataa kurudi England kufanya mazoezi na Chelsea.
Straika huyo mwenye umri wa miaka 28-anafanya juu chini kuwa fiti huku akiwa na matarajio ya kurudi katika timu yake ya zamani ya Atletico Madrid katika dirisha la usajili la Januari baada ya timu hiyo inayoshiriki Ligi ya La Liga kufungiwa kufanya usajili.
Costa alionekana akifanya mazoezi akiwa amevaa bukta ya Chelsea katika video aliyoituma katika Mtandoa wake wa Instagram.

Video hiyo fupi inamuonyesha mfungaji huyo bora wa Chelsea wa msimu uliopita kwa kufunga mabao 20, akifanya mazoezi ya kukimbia katika gym.

Pamoja na kumtaka kurudi, tayari mabingwa hao wa Ligi Kuu wameshaziba nafasi yake kwa kumnasa, Alvaro Morata kwa Pauni 70.6 milioni kutoka Real Madrid.
Morata yuko mbioni kuanza katika kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza wakati timu hiyo itakapoenda uwanjani Wembley kupambana na wapinzani wao wa Mji wa London, Tottenham Jumapili.
Costa ameenda kwenye mji  wa asili yake Brazil baada ya kufukuzwa klabuni Chelsea kwa Ujumbe Mfupi wa Maneno (SMS) na Kocha Antionio Conte. Straika huyo amegoma wito wa Chelsea kutaka arudi London.


Post a Comment

 
Top