0


                     BARCELONA, HISPANIA
BARCELONA imewasilisha ofa mpya ya Uero125 milioni (Pauni 114.2 milioni) ili kumnasa kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho.
Hata hivyo, Liverpool imeikataa ofa hiyo kutoka kwa miamba hiyo ya La Liga na kuendelea na msimamo kuwa nyota huyo hauzwi.
Barcelona inataka kumnyakua staa huyo wa kimataifa wa Brazil baada ya kumuuza Neymar kwenda PSG kwa ada ilivyovunja rekodi ya dunia na imekubali kulipa kiasi kikubwa zaidi ya Euro130 milioni (Pauni118.7m) kumpeleka Coutinho Nou Camp.
Bosi wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema nyota wake huyo hauzwi kwa bei yoyote, pamoja na kwamba Coutinho mwenye umri wa miaka 25-aliwasilisha maombi ya kuhama wiki iliyopita.
Barcelona imefanikiwa kumsaini Paulinho kwa Pauni 36.5 milioni Alhamisi, lakini haitanawa mikono kwa Coutinho, inayemtaka acheze sambamba na Lionel Messi na Luis Suarez Hispania.

Kabla ya ofa hiyo, Liverpool ilikataa ofa mbili kwa ajili ya mchezaji huyo wa zamani wa Inter Milan – zenye thamani ya Pauni 72 milioni na Pauni 90 milioni- na kusisitiza itabakia Anfield katika msimu huu wa dirisha la usajili wa majira ya joto.
Coutinho bado hajaitumikia Liverpool msimu huu baada ya kuumia mgongo akiwa mazoezini. Pia, ataukosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Crystal Palace.  
Alipoulizwa kuhusu uhamisho wa Coutinho baada ya mchezo wa Jumamosi iliyopita dhidi ya Watford ulioisha kwa sare ya mabao 3-3 d, Klopp alikiri kwamba suala hilo kwa sasa haliko mikononi mwake
“Ninaweza kusema jambo moja labda ni muhimu zaidi,” alisema Klopp.
“Kama kocha wa klabu ya soka, nina mabosi wangu. Na kama mabosi wataamua, kwa mfano, muuze mchezaji au hatumuuzi, ninapaswa kukubali.
Coutinho hataki kuichezea Liverpool tena baada ya kuwasilisha maombi ya kuhama kwa njia ya barua pepe kabla ya msimu mpya wa Ligi Kuu.

Post a Comment

 
Top