0


                     MONACO, UFARANSA
PARIS SAINT- GERMAIN (PSG) inakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili straika kinda wa Monaco, Kylian Mbappe kwa Pauni 166 milioni baada ya mazungumzo marefu yaliyomalizika Jumapili.
Katika mazungumzo hayo, PSG inataka kumchukua Mbappe kwa mkopo na italipa pesa msimu ujao wa usajili wa majira ya joto ili kukwepa adhabu ya matumizi mabaya ya fedha.
Mbappe alikuwa katika benchi la Monaco Jumapili na alitarajiwa kwenda Paris, Ufaransa Jumatatu kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya na kusaini mkataba wa miaka mitano.
Mbali na Mbappe, Monaco inaangalia uwezekano wa kumsajili, Stevan Jovetic kutoka Inter Milan ili kuziba mapengo katika sehemu ya ushambuliaji lakini pia inawataka wachezaji wengine pia.
Katika mkutano huo ulioanza jijini Monaco Jumamosi jioni uliwakutanisha baba wa Mbappe, Makamu wa Rais wa Monaco, Vadim Vasilyev, Mkurugenzi wa Michezo wa PSG, Antero Henrique na wakala Jorge Mendes.
Aidha PSG inataka kuwauza baadhi ya wachezaji wake ili kufikia mahitaji yake, ingawaje haitaweza kufanya hivyo hadi katika dirisha la usajili la Januari.
Beki wa pembeni, Serge Aurier anatarajiwa kuuzwa Tottenham kwa dau la Pauni 23 milioni, inatagemea na upatikanaji wa kibali cha makazi, wakati Julian Draxler ana ofa kadhaa kutoka klabu za England.
PSG ineweza kufanya biashara kubwa kwa kuwauza Lucas Moura, Hatem Ben Arfa, Grzegorz Krychowiak, Angel di Maria, Presnel Kimpembe, Adrien Rabiot na Javier Pastore ambao wana ofa kadhaa lakini sio wote watakaouzwa.
Monaco pia, inamuangalia straika Muargeria wa Leicester City, Islam Slimani na pia imeulizia upatikanaji wa straika wa Chelsea, Diego Costa inayemtaka kumchukua kwa mkopo.
Mbappe atakuwa mchezaji wa pili ghali zaidi duniani akitua PSG na atacheza sambamba na mchezaji ghali namba moja, Neymar katika timu moja.



Post a Comment

 
Top