0


                    LEICESTER, ENGLAND
RIYAD MAHREZ (pichani chini) anajipanga kuihama Leicester City katika siku ya mwisho ya usajili Alhamisi baada ya kuruhusiwa kuondoka katika Timu ya Taifa ya Algeria.Timu hiyo ya Kaskazini mwa Afrika ilitoa taarifa katika akaunti yake ya Twitter mapema Alhamisi asubuhi, wakati muda wa mwisho wa usajili ukikaribia. 
Leicester inaamini Mahrez ana thamani ya Pauni 50 milioni, kwa sasa alikuwa akifanya mazoezi na timu ya taifa kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Zambia utakaofanyika Jumamosi.
Katika taarifa yake, Shirikisho la Soka la Algeria limesema: “Mchezaji wa Leicester City, nyota wa kimataifa wa Argeria, Riyad Mahrez, ambaye kwa sasa yuko na timu ya taifa mjini Sidi-Moussa akijiandaa na mchezo dhidi ya Zambia kwa ajili ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018, ameruhusiwa Kocha wa Timu ya Taifa, Lucas Alcaraz na shirikiso la soka la Algeria kwenda Ulaya kumalizia taratibu zake za usajili wa kujiunga na klabu mpya Alhamisi.
“Alhamisi asubuhi kikosi cha timu ya Taifa ya Algeria kitasafiri kwenda Lusaka kucheza na Zambia, mchezo utaopigwa Jumamosi.” 
Winga huyo wa Leicester alitoa mchango mkubwa katika ubingwa wa mwaka 2015-16 – mwanzoni mwa usajili huu wa majira ya joto alitajwa kujiunga na Roma ya Italia lakini dili hilo lilikufa.
Klabu hiyo inayocheza Ligi ya Serie A ilishuhudia ofa zake tatu za kutaka kumtwaa zikikataliwa na Leicester.
Wakati huohuo, Gazeti la Michezo la Hispania AS limeandika Barcelona imemfahamisha Mahrez inamhitaji baada ya kukwama kumtwaa Philippe Coutinho kutoka Liverpool.
Liverpool imekataa kumuuza Mbrazili huyo, ambaye kwa sasa anajianda na mchezo wa Alhamisi wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Ecuador, kwa kukataa ofa tatu – ikiwemo kubwa zaidi ya Pauni 114 milioni. 
Gazeti la AS limeripoti pia Arsenal inaweza kumpoteza Alexis Sanchez kwa Manchester City siku ya mwisho ya usajili.
City inaweza kurudi kwa Gunners na ofay a Pauni 70 milioni kwa ajili ya Mchile huyo baada ya ofa yao ya pauni 50 milioni kukataliwa na klabu hiyo ya Kaskazini mwa London. 


Post a Comment

 
Top