LIVERPOOL,
ENGLAND
TAKATAKA
kabisa. Ndiyo, bora waseme wao kuliko wengine. Wachambuzi mahiri wa soka, huku
wawili kati yao wakiwa wameichezea Arsenal kwa mafanikio, wameibuka na kuiponda
klabu hiyo baada ya kichapo walichochezea kutoka kwa Liverpool.
Thierry
Henry na Martin Keown ambao wameichezea Arsenal kwa mafanikio chini ya utawala wa
Kocha wa sasa, Arsene Wenger wameungana na beki wa zamani wa Manchester United,
Gary Neville kuponda kiwango kilichoonyeshwa na Arsenal.
Wababe
hao wa Jiji la London, Jumapili waliendeleza mdororo wao wa miaka ya karibuni
baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Liverpool katika Uwanja wa
Anfield huku wakionyesha moja kati ya viwango vibovu katika utawala wa Kocha
Wenger.
“Nilitaka
kuondoka uwanjani. Sifanani na hiyo timu na nilikuwa natazamia hilo. Wakwame.
Nilijua hilo lingetokea tu leo, lakini bado unapoona mambo yanakwenda hivyo,
unasema hapana, isitokee tena jamani. Hata hivyo, sishangazwi sana,” alisema
Henry.
“Namna
ambavyo Arsenal wanapoteza mechi ni tatizo. Tunaongelea kuhusu hamu ya timu na
kujitolea kupambana. Inaumiza sana na namna wanavyopoteza mechi ni vilevile tu.
Kama shabiki unajaribu kujipa moyo, lakini sio kitu kizuri kuona. Nini kingine?
Kila unachokiona leo kimekuwa kikitokea kwa miaka 10 iliyopita,” alilalamika
Henry.
Naye
Keown, ambaye alikuwa beki nguli enzi zake alihoji mbinu za Wenger kuelekea
katika pambano hilo huku akishangaa kwanini alimuacha nje mshambuliaji wake
aliyemnunua kwa pesa nyingi, Alexandre Lacazette na kumpanga Danny Welbeck.
Bao la kwanza lilifungwa na Roberto Firmino
“Najaribu
kukumbuka ni lini Arsenal walicheza kiwango kibovu kama hiki. Ni udhalilishaji.
Hawa ni wachezaji ambao wanaonekana kama vile hawataki kuwa hapa. Na kocha
anaonekana kama vile amepotea njia yake,” alisema Keown.
“Sioni
kama Arsene Wenger anafanya maamuzi sahihi. Kwanini alimuacha nje Alexandre
Lacazette aliyenunuliwa kwa rekodi ya klabu Pauni 53 milioni katika mechi
muhimu kama hii? Ingeleta maana kumchezesha katika uwanja ambao Arsenal
haijashinda kwa miaka mitano,” aliongeza Keown.
Maneee!
“Kwanini
Hector Bellerin alichezeshwa kama beki wa kushoto wakati Sead Kolasinac, ambaye
ni beki wa kushoto asilia alikuwepo? Kolasinac amecheza vizuri katika mwanzo
huu wa msimu. Kwanini Gabriel ameuzwa? Beki, ambaye ana nguvu sambamba na Laurent
Koscielny. Ina maana Rob Holding ambaye hana uzoefu, ameingia katika kikosi cha
kwanza Aprili alirushwa kwa Mbwamwitu.”
Naye
Neville, ambaye anajulikana kwa kuichukia Liverpool akiwa mchezaji wa United
alidai, wachezaji wa Arsenal hawastahili kuvaa jezi za timu hiyo.
Sanchez akifuatilia mchezo baada ya kutolewa
“Ni
kitu kilichosemwa sana kwamba mimi sio shabiki wa Liverpool, lakini timu hii ya
Arsenal ilistahili kuchapwa. Walistahili kabisa. Liverpool ni wazi katika
kwenda mbele, lakini unawezaje kucheza hivi katika mechi kubwa na wachezaji
kama wa Arsenal?” alihoji Neville.
Salaaaah!
“Achana
na habari ya kutojituma, achana na habari ya kucheza vibaya, lakini kiukweli
wana tabia ya kukosa heshima kwa jezi. Wachezaji watatu hadi wanne wanashindwa
kukimbia wala kujali, ni fedhea kwa klabu kubwa. Nilikuja nikiwa nimetulia leo
lakini kwa kweli nimekasirika na nina hasira na sijui mashabiki wao
wanajisikiaje,” aliongeza Neville.
Wakati
huo huo, Henry alirudi tena kuonyesha wasiwasi kama Alexis Sanchez anaweza
kubakia tena klabuni hapo baada ya matokeo ya mechi ya Jumapili.
Sturridge akishangilia la nne
“Tunaongea
suala la Sanchez na kwamba anabakia, lakini hawezi kutaka kuwa sehemu ya timu
hii. Na ndio maana wachezaji hawasaini mikataba mipya, kuna kitu wanakiona
hakipo sawa,” aliongeza Henry, ambaye mpaka sasa ndiye mfungaji bora wa muda
wote katika kikosi cha Arsenal.
Post a Comment