0


                             LIVERPOOL, ENGLAND
ALEX OXLADE-CHAMBERLAIN amepigwa picha akiwa na jezi ya Liverpool kwa mara ya kwanza tangu alipokamilisha usajili wa Pauni 35 milioni kutoka Arsenal.
Nyota huyo mwenye umri wa mika 24-alifanyiwa vipimo vya afya na kukubali dili la miaka mitano lenye thamani ya Pauni 120,000 kwa wiki ili kujiunga na vijana wanaongozwa na Kocha Jurgen Klopps Jumatano.
Kisha Liverpool ikathibitisha kuwasili kwa staa huyo kutoka London Kaskazini kupitia akaunti ya Twitter, ikituma ujumbe mwepesi wa kumkaribisha sambamba na picha ya kikosi.
Akiwafahamisha mashabiki wa Liverpool kwa mara ya kwanza baada ya kuhama, Oxlade-Chamberlain alinukuliwa na Mtandao wa Liverpool: “Kwa sasa niko nje ya kambi ya England, nipo St George's Park. 
                                                                ...akiwa na jezi ya Liverpool
...akifanyiwa vipimo vya afya
“Kwanza, nina furaha ya kujiunga na Liverpool na namshukuru kila mmoja hapa katika Chama cha Soka (FA) kufanikisha hili, kutumia vifaa. Ni msaada mkubwa sana.
“Sitasema mengi leo; niko hapa na timu ya taifa na tutacheza michezo miwili mikubwa, kwa hiyo ninataka kuweka akili yangu kwenye michezo hiyo. Lakini siwezi kusubiri kufika Melwood na mtanisikia kupitia Liverpool TV.”


Post a Comment

 
Top