BARCELONA,
HISPANIA
LIONEL
MESSI sasa ameazimia kuihama Barcelona baada ya miamba ya Ligi Kuu England, Manchester City kufanya
kikao na wawakilisha wa mchezaji huyo.
Messi
ambaye amefunga mabao 508 katika michezo 585 aliyoitumikia Barcelona tangu
mwaka 2004, pia ameisaidia timu hiyo kutwaa mataji manane ya La Laliga na manne
ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huku akijijenga kuwa mmoja kati ya wachezaji wakubwa
kwa muda wote klabuni hapo.
Straika
huyo mwenye umri wa miaka 30-alionekana kukubali kujifunga kwa muda mrefu Barcelona
kwa kukubali mkataba wa miaka minne mwezi uliopita, lakini ripoti zinasema
uhamisho wa kushangaza katika majira haya ya
joto unaweza kutokea.
Habari
zinasema, mkutano kati ya viongozi wa Manchester City na wawakilishi wa Messi
ulifanyika jijini Barcelona wiki iliyopita, na klabu hiyo ya Ligi Kuu England
ikaulizia uwezekano wa Muargentina huyo kutua England.
Inadaiwa
Messi anazidi kuchanganyikiwa na hali inayoendelea Barcelona- kufuatia mchezaji
mwenzake na rafiki yake Nemar kuuzwa Paris Saint-Germain (PSG) mwezi uliopita pamoja
na viongozi wa Barcelona kusisitiza kwa asilimia ‘200’ angebaki.
Barcelona
inahangaika kutaka kumsajili mbadala wa Neymar, kutoka Liverpool, Philippe
Coutinho ambaye klabu yake imesema hauzwi. Tayari Barca imepeleka ofa tatu na
zote zimekataliwa.
Pia,
Messi anazidi kuchanganyikiwa na matokeo ya uwanjani baada ya timu yake kupata
vipigo viwili mfulululizo kutoka kwa mahasimu wao, Real Madrid katika mchezo wa
Hispania Super Cup.
Mchezo
wa kwanza ilifungwa mabao 3-1 katika uwanja wa nyumbani wa Camp Nou na ule wa ugenini
uliofanyika Bernabeu ilifungwa 2-0.
Man
City imeonyeshwa kuvutiwa na Messi kwa miaka kadhaa sasa na Kocha Pep Guardiola
ana matumaini ya kumsajili fowadi mwingine kabla ya dirisha la usajili kufungwa
Agosti 31.
Straika
wa Arsenal, Alexis Sanchez amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa kutua Etihad
lakini Arsenal na kocha wake, Arsene Wenger hawana mipango ya kumuuza raia huyo
wa Chile katika msimu huu wa majira ya joto.
Post a Comment