LIVERPOOL, ENGLAND
TOM WERNER
(pichani juu) amesisitiza katika siku muhimu ya historia ya Liverpools kwamba Fenway Sports Group (FSG) haiko
kwa ajili ya kuiza klabu hiyo.
Werner, ambaye ni
Mwenyekiti wa Liverpool, alikuwa uwanjani Anfield Ijumaa sambamba na mmiliki
mkuu, John W Henry na Rais wa FSG, Mike Gordon katika ufunguzi wa jukwaa lenye
thamani ya Pauni115 milioni, ambalo litaongeza uwezo wa uwanja huo kubeba watu 54,000.
...jukwaa lililojengwa Anfield
Jurgen Klopp(kushoto) anategemea timu kupata faida zaidi.
“Mchezo wa Jumamosi
dhidi ya Leicester City umeuzwa lakini kuuza siyo sera ya FSG,” alisema Werner.
Kumekuwapo na maneno
kuhusu kampuni ya Kichina katika majira haya ya joto lakini Werner amesisitiza
siyo yeye wala washirika wake wanaoangalia suala hilo la fedha.
Kikosi cha Liverpool kikifanya mazoezi Anfield.
“Nimeshasema mara kwa mara, hii klabu haiuzwi,”
Werner alisema. “Sijui ninaweza kusema mara ngapi jambo hilo. Tunatambua hii ni
changamoto, siyo kwa ajili yetu bali kwa mashabiki wetu, na kwetu ili
kushindana kwenye ngazi za juu tunatakiwa kuja na ufumbuzi.
Matajiri wa Kichina
walikuwa wakiitolea macho klabu hiyo na kutaka kuinunua na kuifanya kuwa tajiri
kuliko Manchester City.
Post a Comment