LEICESTER,
ENGLAND
CLAUDIO RANIERI
(pichani juu na chini) amewaambia wachezaji wake kwamba hakuna mwenye uhakika wa namba katika kikosi
hicho katika kipindi hiki cha majira ya joto ambapo Leicester imejipanga kujiimarisha.
Leicester imewaongeza
wachezaji wapya sita katika kutetea taji lake na Kocha Ranieri amesisitiza kuwa
hiyo inamaanisha hakutakuwa na nafasi ya kudumu hata kwa upande wa wachezaji
wakubwa.
Kocha huyo wa Leicester
msimu uliopita alikuwa ni nadra sana kubadilisha kikosi chake wakati akisaka taji
la England, alikijenga kikosi chake kupitia wachezaji 10 wakiwamamo Jamie
Vardy, Riyad Mahrez na Danny Drinkwater katika michezo 30.
Lakini sasa ana uchaguzi mpana baada ya kuwasili kwa Islam Slimani, Ahmed
Musa, Nampalys Mendy, Bartosz Kapustka, Luis Hernandez na Ron-Robert Zieler, na
kikosi chake kimekuwa na changamoto.
“Bila shaka hakuna
uhakika wa kudumu,”alisema Muitaliano huyo. 'Hakuna kesi kwamba kwa sababu fulani
alicheza msimu uliopita ana uhakika wa kucheza msimu huu. Ninaangalia kila
mazoezi, naangalia kila mechi, na kama nakimuona mtu ni bora, nabadilisha
kikosi.
“Hakuna mwenye uhakika wa kuvaa jezi na kuanza katika kikosi. Kila mmoj anatakiwa kuwa katika kiwango cha juu na kama mtu atashuka nitakuwa na mtu wa kumbadilisha. Hilo ndilo muhimu.
“Hakuna mwenye uhakika wa kuvaa jezi na kuanza katika kikosi. Kila mmoj anatakiwa kuwa katika kiwango cha juu na kama mtu atashuka nitakuwa na mtu wa kumbadilisha. Hilo ndilo muhimu.
Slimani amejiunga na Leicester kwa Pauni 29.7.
“Mwishoni siyo kikosi
cha wachezaji 11 watakaokuwa wametwaa ubingwa, ni wachezaji wote, wote ni
mabingwa katika Premier League. Sikumbuki nani amecheza michezo 38 na nani
amecheza mchezo mmoja. Kwangu ni kundi lote limetwaa ubingwa.”
Leicester mazoezini
Jumamosi hiii, Ranieri ataingoza
Leicester uwanjani Anfield na anamini
wachezaji wake wanaweza kushinda kutokana na presha waliyonayo Liverpool ya
kupata ushindi baada ya kufungua jukwaa jipya uwanjani hapo.
“Wamecheza michezo
mitatu nje na huu ni wa kwanza nyumbani. Watakuwa na wasiwasi wa kuonyesha
ubora wao,” alisema Ranieri.
Ranieri
“Watakuwa na wasiwasi
wa ushindi. Lakini hawakuwa na uhakika wa ushindi. wanaweza, lakini pia Leicester
inaweza kushinda.”
Mbali na mchezo dhidi
ya Liverpool, Leicester utaanza kucheza Ligi ya Mabingwa kwa kusafiri kuifuata Club
Brugge wiki ujayo lakini Ranieri amekiri wachezaji wake hawaaanza kuyafikiria
mashindano hayo.
Post a Comment