0


MANCHESTER, ENGLAND
WAYNE ROONEY ameachwa katika kikosi cha wachezaji 20 cha Manchester United kitakachocheza Europa League dhidi ya Feyenoord Alhamisi.
Mbali na Rooney, kiungo Henrikh Mkhitaryan na straika, Jesse Lingard ambao walicheza Jumamosi dhidi ya Manchester City uwanjani Old Trafford, pia hawatasafiri kwenda  Uholanzi.

Mourinho
Kikosi hicho kilitangazwa kwenye Mtandoa wa Manchester United mapema.

Rooney
Mkhitaryan alipangwa katika mchezo huo wa upinzani ambapo Man United ilifungwa mabao 2-1 pamoja na kwamba alikuwa akisumbuliwa na  majeraha ya paja baada ya kumaliza mchezo wa kimataifa wa kuitumikia Armenia na  Kocha wa United, Jose Mourinho alitarajiwa kuliweka wazi hilo katika mkutanono wake na waandishi wa habari Jumatano.

Ibrahimovic
Kiungo huyo hakuwepo katika mazoezi ya timu hiyo sambamba na kikosi cha Manchester mapema Jumatano.
Mabeki ambao wamekuwa na desturi ya kuanza kwenye kikosi cha United, Antonio Valencia na Luke Shaw, pia wameachwa- huku wadau wakidai kwamba nafasi kubwa itakuwa kwa Matteo Darmian, Marcos Rojo na Tim Fosu-Mensah.

Post a Comment

 
Top