0
JOSE MOURINHO amekiri kwamba alitakwia kuingiza timu tofauti na ile iliyopokea kichapo cha mabao 2-1 katika uwanja wa nyumbani dhidi ya wapinzani wao Manchester City Jumamosi.
Kocha Mourinho aliwaanzisha Henrikh Mkhitaryan na Jesse Lingard na kuwaacha nje Anthony Martial na Juan Mata. Wote wawili Mkhitaryan na Lingard aliwabadilisha kipindi cha pili  baada ya City kutawala mchezo.

Mkhitaryan 
Mourinho alisema: "Kwa kusema kweli, nilikuwa na wachezaji wawili au watatu ambao kama ningejua kile ninachokijua, nisingewachezesha. Lakini hili ni soka. Kuna wakati wachezaji wanawaangusha makocha. Wakati mwingine wanafanya maajabu.
"Hawakunipa kile nilichotaka. Ni makosa yao na kosa langu kama kocha."
United ilishafungwa mabao 2-0 yakipachikwa na Kevin De Bruyne na Kelechi Iheanacho kabla ya Zlatan Ibrahimovic kufunga bao la kufutia machozi kutokana na makosa ya kipa wa City, Claudio Bravo.

Lingard 
Akiuzungumzia mchezo huo Mourinho aliongeza: "Katika kipindi cha kwanza, walicheza vizuri. Tulianza mchezo vibaya. Baadhi ya wachezaji walicheza chini ya kiwango. Tunahitaji kuwa mashapu. Timu inalipa kwa ajili hiyo.
"Kipindi cha pili kilikuwa tofauti kwa kiasi kikubwa. Walipomuingiza Fernando haraka, ni kwa sababu walijua tulikuwa tumewamudu na kuwa hatari zaidi."
Katika mkutano wa waandishi wa habari, Mourinho aliongeza: " Sikutaka kufanya mabadiliko ndani ya dakika 20 kwa sababu sikutaka kuwakatisha tamaa wachezaji. Mapumziko, tulibadilisha mwelekeo wa mchezo lakini hatukuweza kupata fidia inayostahili kipindi cha pili.
"Hatukuweza kuwadhibiti (katika kipindi cha kwanza) na timu haikuwa na maendeleo – na ni vigumu kucheza vizuri kwa maneno ya kwenye mstari wa pembeni. Katika kipindi cha kwanza, tulifanya makosa mengi."

... Mourinho akitoa maagizo
Kocha Mourinho pia alisema baadhi ya wachezaji wake walishindwa kufuata maelekezo yake, ukimtoa beki Eric Bailly, ambaye amekuwa akivutia United hadi kwenye derby hiyo.

Kocha huyo wa United alifafanua: "Nini nilichowaambia wakati wa mapumziko 'baadhi yenu, inaonekana mnajaribu kufanya kile nilichowaambia msifanye.' Nilimwambia (Eric) Bailly kutocheza baadhi ya mipira- kamwe. Alifanya hivyo mara 20 katika mchezo. Baadhi  waliuona mwelekeo wa mchezo."

Post a Comment

 
Top