PARIS, UFARANSA
WAGNER RIBEIRO mmoja kati ya mawakala
wa Neymar (pichani) amefichua kwamba Mbrazili huyo amekataa ofa nono za Rais wa Klabu ya Paris
Saint-Germain, Nasser Al-Khelaifi katika kipindi cha usajili cha majira ya joto
kabla ya kukubali kuongeza mkataba wake na Barcelona.Neymar 24, amejifunga katika dili la miaka mitano lililoanza Julai na Barca, lakini Ribeiro ameweka wazi kwamba mteja wake angepata kiasi kikubwa cha fedha kama angejiunga na mabingwa wa jijini Paris.
... akifanya yake uwanjani.
Kwa mujibu wa Ribeiro, Rais wa PSG, Nasser amekutana na mchezaji huyo kwa
siri mara mbili akiwa na baba yake katika Kisiwa cha Ibiza mwanzoni mwa Juni na
mara nyingine walikutana Brazil baadaye ndani ya mwezi huohuo."Ni miye ndiye niliyempeleka Nasser jijini Sao Paulo," alisema katika mahojiano haya yaliyofichua mambo mazito.
"Nilimwambia ofa hiyo haikuwapo duniani; kwamba angekuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani na kusingekuwana mchezaji anayelipwa zaidi yake.
...Neymar
"PSG ilikuwa tayari kulipa
(Uero190 milioni kima kinachotakiwa katika kifungu kilichokuwa kinamruhusu
kuondoka) na angepata Uero 50 milioni (Pauni 42 milioni) kwa mwaka baada ya
kukatwa kodi. Tulizungumza kwa saa mbili na Neymar alishakuwa na shauku. Nasser
alifafanua kwamba hakutakuwa na matatizo ya kodi PSG na mchezaji huyo angekuwa No.
1 katika timu tofauti na Barca."
Ribeiro
Mbali na mshahara huo mnono, Ribeiro
pia alidai Al-Khelaifi alimpa Neymar ofa ya ndege binafsi ya kusafiria kwa
ajili ya michezo ya Brazil na shea katika mlolongo mpya wa hoteli kwa jina lake
– kama ilivyo kwa Cristiano Ronaldo. Hata hivyo, Neymar ambaye shughuli zake nyingi zinasimamiwa na baba yake kuliko wakala wake, aliamua kubaki Barcelona, pamoja na kwamba aliridhika na juhudi zilizofanywa na mabingwa hao wa Ligue 1.
"Kama amebaki ni kwa sababu ana furahia maisha ya Barcelona, na na jiji lake," Ribeiro alisema.
"Nilimtaka ajiunge na PSG, lakini baba yake alipendekeza abaki.
Neymar akiwa na rafiki yake.
"(Kama angeondoka) ingekuwa ni
kwa ajili ya PSG, kwa sababu rais amezungumza moja kwa moja naye, kitu ambacho
hakijafanywa na (Rais wa Real Madrid), Florentino (Perez) wala Manchester
United."Ribeiro aliwahi kutoa madai kadhaa kuhusu nia ya PSG kumtaka Neymar, lakini madai hayo yamekuwa yakikemewa na klabu hiyo.
... akipiga kinanda.
Kikizungumza na Gazeti la L’Equipe, chanzo
kutoka ndani ya PSG kimedai kwamba hakuna ukweli katika stori ya Wagner."Moja kwa moja ni uongo," chanzo hicho kilisema. "Pamoja na mchango wa mwajiri kuwa juu, mshahara huo unaweza kugharimu zaidi ya Euro 60 milioni kwa mwaka. Neymar alitumika kwetu kuongeza nguvu yake Barcelona."
Gazeti hilo la michezo la kila siku liliongeza kwamba, hata hivyo, Naibu Mkurugenzi wa Michezo wa PSG, Olivier Letang alikwenda Brazil mwishoni mwa Juni kukutana na wasaidizi wa Neymar.
Post a Comment