0



MANCHESTER, ENGLAND
VITA ya maneno makali kati ya wakala wa Yaya Toure, Dimitri Seluk na Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola vinaonesha hakutakuwa na muafaka kati yao.
Wakala huyo wa Toure amekataa kumuomba radhi Guardiola na kudai kwamba Mhispania huyo alikuwa na mchanga mdogo sana katika mafanikio ya Barcelona alipokuwa kocha.
Guardiola kushoto na Yaya Toure
Seluk ameibuka tena mbele ya jamii, saa 24- baada ya Guardiola kumtaka raia huyo wa Ukraine kumuomba radhi kutokana na maneno yake kuhusu Manchester City.
Picha ya Kikosi cha City bila ya Yaya.
 Wakila huyo wa muda mrefu wa Toure, mteja wake amesimamishwa chini ya Guardiola ambaye amesema hataichezea City tena hadi Seluk atakapoomba radhi.
Hata hivyo, Seluk ameongeza petroli kwenye moto kwa kudai kwamba kiwango cha Barca kutamba Hispania na Ulaya kimejengwa chini ya Kocha, Frank Rijkaard na Lionel Messi– na sio bosi huyo wa sasa wa Etihad. 

“Barcelona imejengwa na Rijkaard na baadaye (Guardiola) alikuwa na bahati kwa kuwa alikuwa na Messi,” Seluk alisema. 
“Ni Messi ambaye ameijenga Barca, siyo Pep. Kocha Luis Enrique ameonyesha mafanikio ya Barca hayakua chini ya Guardiola. 
Kocha Guardiola alishinda mataji matatu ya La Liga na mawili ya Ligi ya Mabingwa wakati alipiokuwa Nou Camp, na kufuatia na mataji matatu mfululizo ya Bundesliga, lakini  Seluk amehoji asili ya ushindi huo. 

“Hata pale Munich. Asingeweza kufeli. Babu yangu angeweza kushinda taji la ligi akiwa na timu hiyo,” alisema. 
“Kama Pep anataka kujiaminisha kwamba yeye ni kocha mkubwa, aende Zaragoza au Sunderland. Tutaona ni mzuri atakapoacha kuchukua timu kubwa na akiwa hapati pauni nusu bilioni za kutumia kununua wachezaji.” 
Jumanne hii, Seluk alikubali kuingia vitani kupambana na Guardiola kwa jinsi anavyomtendea Toure ndani ya City tangu Mhispania huyo alipowasili Etihad.

Seluk kushoto na Toure.
Awali, raia huyo Ukraine alilamikia mteja wake raia wa Ivory Coast kunyanyaswa kwa kuachwa katika kikosi cha Ligi ya Mabingwa, wakati Toure akiwa amecheza mchezo mmoja tu chini ya Guardiola – mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Steaua Bucharest katika mchezo ambao kocha huyo wa City aliwapanga wachezaji damu changa kama Pablo Maffeo, Tosin Adarabioyo na Angelino.
Kinachouma zaidi, mchezaji huyo bora mara nne wa Afrika hajajumuishwa katika picha ya pamoja ya klabu, ambayo iliachiwa  kwenye mitandao Jumanne.

Picha hiyo ilipigwa wakati Toure alipokuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kipanda uso.
Uamuzi wa kuendelea kufanya maamuzi hayo bila ya uwepo wake, unazungumzwa ni kutokana na kuongezeka kwa uadui kati wakala na kocha wake. 
Seluk alisema: “Pep hawataki wachezaji wanaojitambua. Anawataka wachezaji wanaomuogopa na wanaofanya kile anachokisema.
“Kitu cha kwanza alichokifanya alipowasili City ni kuwaondoa Yaya na Joe Hart, wachezaji wawili wakubwa klabuni. Wote wanaheshima kubwa katika vyumba vya kubadilishia nguo klabuni Man City na Guardiola hakulipenda hilo.”
Wakala huyo alimtaka Guardiola  kumwomba radhi kipa Joe Hart na bosi wa zamani wa City, Manuel Pellegrini kwa kuingilia kibarua chake Etihad.

Wakati sasa kukiwa na msuguano huo na Toure amebakisha miezi minane ya kuendelea na dili lake la kulipwa  Pauni 225,000-kwa wiki klabuni hapo. 
Licha ya mkataba wake kumruhusu kuendelea, Yaya Toure ataondoka katika dirisha la usajili la Januari.
Hata hivyo, kiungo huyo anataka kubaki Ligi Kuu England na baadhi ya klabu kubwa za Manchester United, Arsenal, Liverpool na Chelsea zimeonyesha nia ya kumtwaa.  
Seluk alisema :“Guardiola ameshinda michezo michache na anajiona mfalme,” Seluk alisema.

Post a Comment

 
Top