LONDON, ENGLAND
JOSE MOURINHO na Pep
Guardiola wamepangwa kukutana tena katika Manchester derby katika raundi ya nne ya Kombe la Ligi (EFL)uwanjani Old Trafford mwezi ujao.
Makocha hao
wamepangwa kukutana siku 11 baada ya Guardiola wa Manchester City kuibuka na
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester United ya Mourinho katika mchezo wa Premier
League.
Ratiba ya EFL
itaikutanaisha miamba mingine ya Ligi Kuu ya Premier League, Liverpool itakapoikaribisha
Tottenham Hotspur na Chelsea itapambana na wapinzani wao wa London West Ham
United.
Norwich ambayo
iliifunga Everton uwanjani Goodison Park itasafiri kwenda Elland Road kucheza
na Leeds wakati Preston iliyoifunga timu ya Premier League ya Bournemouth, itaenda
Newcastle.
Miamba mingine ya
Premier Leagua, Arsenal itakuwa wenyeji wa Reading wakati Hull City itasafiri
hadi Kusini Magharibi kucheza na Bristol City.
Na kutakuwa na
pambano lingine la timu za Premier League kati ya Southampton na Sunderland.
Ratiba
ya raundi ya nne ya EFL Oktoba 24:
West Ham United
|
v
|
Chelsea
|
Manchester United
|
v
|
Manchester City
|
Arsenal
|
v
|
Reading
|
Liverpool
|
v
|
Tottenham Hotspur
|
Bristol City
|
v
|
Hull City
|
Leeds United
|
v
|
Norwich City
|
Newcastle United
|
v
|
Preston North End
|
Southampton
|
v
|
Sunderland
|
Post a Comment