MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO (pichani chini) ameibuka na visingizio
akidai kuwa wachezaji wake bado
wanasumbuliwa na mbinu za aliyekuwa mtangulizi wake, Louis van Gaal.Kauli hiyo ya Mourinho imetolewa baada ya kuishuhudia timu yake ikipoteza mechi tatu mfululizo za mashindano tofauti Ulaya.
Mourinho aliwaeleza marafiki zake kwamba vipigo hivyo vimechangiwa na wachezaji wake kuweka akili zao kwenye miaka miwili ya aliyekuwa kocha wao, Mdachi Van Gaal ambazo zilikuwa hazieleweki.
Kocha huyo Mreno ameshikilia msimamo kuwa kumbukumbu ya Van Gaal bado inawatesa wachezaji wake kwenye kikosi cha Manchester United.
Kwa sasa, Mourinho anakabiliwa na janga la wachezaji wake kucheza vibaya, baadhi yao kutojiamini, kukosa mabao na hata kushindwa kulinda lango lao.
Matokeo yake, Mourinho anaamini kuwa jinamizi la Van Gaal ndiyo sababu ya msingi ya wachezaji wake kufanya vibaya.
Alidai kuwa anahisi wachezaji wake bado wanaamini kwenye mbinu za mtangulizi wake za kutotaka mabadiliko katika uchezaji wao.
Mourinho aliwahi kufanya kazi chini ya Van Gaal kwenye Klabu ya Barcelona kwa miezi mitatu alipoanza kazi ya ukocha.
Van Gaal
Alieleza imani yake kubwa ni
kuwabadili kimtazamo wachezaji wake wasahau miaka miwili ya maisha chini ya
Mdachi yule ambaye kwa sasa hana timu.Pia, kocha huyo amemkosoa beki wake, Luke Shaw kwa bao la pili dhidi ya Watford, Jumapili walipofungwa 3-1 kwenye Uwanja wa Vicarage Road, akaeleza mshangao kwa jinsi mabeki wake wanavyojipanga dhidi ya wapinzani wakati wa mashambulizi.
Mourinho alieleza kuwa amekuwa akiwashauri waende mbele kusaidia mashambulizi, lakini baada ya miaka miwili chini ya LVG ambako waliambiwa wabaki nyuma hawataki kufanya wanaloambiwa.
Kocha huyo, maarufu ‘The Special One’ anaeleza kuwa baadhi ya wachezaji wake wamechanganyikiwa, jambo ambalo limechangia vipigo katika mechi tafu mfululizo, ambako Jumatano ilicheza dhidi ya timu ndogo ya Northampton kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya Kombe la Ligi na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Inaaminika kuwa kiungo wake, Ander Herrera amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa nyota walioathiriwa na falsafa ya Van Gaal.
Mourinho
Hata hivyo, Mourinho anaamini kuwa
wachezaji wake watazishinda tabu hizo na kukubaliana na mfumo wake wa uchezaji
ambao amekuwa akiwapa tangu atue Old Trafford.
Post a Comment