0


MANCHESTER, ENGLAND
MANCHESTER UNITED imeripotiwa kuwa tayari kumlipa mishahara yake yote kiungo wake wa Kijerumani, Bastian Schweinsteiger – yenye jumla ya thamani ya Pauni 13.8 milioni- ili kumwachia aondoke zake Old Trafford.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32-amekuwa haihitajiki katika kikosi cha Kocha Jose Mourinho na amelazimishwa kufanya mazoezi na kikosi cha wachezaji wa akiba.
Pamoja na kwamba Mjerumani huyo amebakisha miaka miwili katika mkataba wake, Mourinho amemuweka wazi kwamba  hahitajiki United.

Habari ndani ya Old Trafford, zinasema, Schweinsteiger alitaka kulipwa mabaki ya mshahara wake kwa jumla kama Old Trafford inataka aondoke.
Akiwa amebakisha miezi18 na anapokea Pauni150,000- kwa wiki kwa mujibu wa mkataba wake, inaweza kuigharimu United kama Pauni 13.8 milioni kumlazimisha mchezaji huyo kuondoka lakini klabu inakaribia kufanya makubaliano na wawakilishi wa  mchezaji huyo.
Mchezaji huyo alibaki Manchester katika kipindi cha dirisha la usajili la majira ya joto kwa sababu ya mshahara wake mkubwa na timu kadhaa kushindwa kumsajili.
Lakini kama malipo hayo yatakuwa yameafikiwa  kati ya Schweinsteiger na United, mchezaji huyo wa zamani wa Bayern Munich ataweza kuwa huru kucheza katika miaka yake ya mwisho katika klabu mpya- kinyume na anavyoteseka United kwa kutupwa kwa wachezaji wa akiba.
Inafahamika kwamba anaweza kufungua milango ya kwenda kucheza Ligi ya Marekani Major League kufuatia kauli yake aliyoitoa Agosti akithibitisha kwamba United itakuwa klabu yake ya mwisho barani Ulaya.
Pamoja na kufedheheshwa na kutengwa na Mourinho, Schweinsteiger hajafungua  mdomo wake na kuiponda klabu hiyo na hata alionyesha nia yake ya kutembelea tena Old Trafford kabla ya kuondoka klabuni.

Post a Comment

 
Top