0


LONDON, ENGLAND
ARSENE WENGER amesema hana mpango wa kukisoma kitabu kipya cha Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho kiitwacho ‘Jose Mourinho: Up Close and Personal’, ambacho kimejumuisha maneno mengi ya dharau dhidi yake.
Kitabu hicho kimeandikwa na Mwandishi wa Habari, Rob Beasley ambaye amekuwa akifanya kazi karibu na Mourinho, akinukuu madai kwamba mwaka 2014, Mourinho alisema: “Siku moja nitamtafuta (Wenger) nje ya uwanja na kuuvunja uso wake.”

Wenger (kushoto) Mourinho (kulia)
Bifu la Mourinho na Wenger lilirudi upya wakati Mreno huyo aliporejea Chelsea mwaka 2013, ambapo makocha hao kila mmoja alionyesha ubabe kwa mwenzake, ikiwamo tukio la kukunjana mashati kwenye moja ya mechi zao.
Wenger anaripotiwa kuchukizwa na Mourinho baada ya kumuuza Mhispaniola, Juan Mata kwenda Manchester United na kumtuhumu kwamba anauzia maadui silaha kwa kuwa yeye ameshacheza nao. Jambo hilo liliibua malumbano na Mourinho kutoa kauli ya kumpasua Wenger.
Alipoulizwa maoni yake juu ya tishio hilo, Wenger alicheka na kusema: "Sijakisoma kitabu hicho na bila shaka sitakisoma. Kwa hiyo sitaweza kutoa maoni yangu.

... wakiamuliwa.
"Ninazungumza kuhusu soka na hicho ndicho nitakachokifanya. Mimi si mharibifu, hapana. Nipo kwa ajili ya kujenga na siwezi kutoa maoni kama hayo, kwa sababu ninaangalia zaidi mchezo dhidi ya Chelsea na jinsi ninavyotaka tucheze."
Kocha Mourinho aliwahi kumpachika Wenger jina na kumwita ‘Bingwa wa Kufeli’ miaka miwili iliyopita na mwaka 2015 walitaka kushikana mashati wakati bosi huyo wa Arsenal alipomsuka kifuani Mourinho katika mchezo ambao Gunners ilifungwa mabao 2-0 uwanjani Stamford Bridge.
Pia, Wenger aliulizwa kama anadhani uhusiano wake na Mourinho unaweza kuwa mzuri siku moja – kama ulivyokuwa  upinzani wake wa zamani na Sir Alex Ferguson - alisema: "Siku zote ndivyo unavyoisha kama hivyo.
“Sina matatizo binafsi na mtu yeyote. Ninamheshimu mtu yeyote kwenye mchezo.

Kocha Wenger
Kocha Wenger atacheza dhidi ya Kocha wa Chelsea, Antonio Conte kwa mara ya kwanza uwanjani Emirates Jumamosi, lakini Wenger alisema anahisi upinzani mkali umepungua tangu kuondoka kwa Mourinho klabuni Chelsea.

Post a Comment

 
Top