LYON, UFARANSA
EMMANUEL ADEBAYOR
ameponda madai kuwa aliagiza pombe aina ya whisky na alikuwa akivuta sigara
alipokutana na mwakilishi wa mwakilishi wa klabu Lyon ya Ufaransa kwa ajili ya
mazungumzo ya kujiunga na klabu hiyo.
Straika huyo wa
kimataifa wa Togo mwenye umri wa miaka 32- ambaye kwa sasa hana klabu baada ya
kuachwa na Crystal Palace katika usajili wa majira ya joto alikutana na klabu
hiyo ya Ligue 1 wiki iliyopita jijini Lyon.
Adebayor aliwahi kuitumikia Real Madrid
Adebayor alisema,
uhamisho huo ulishindikana kwa sababu Lyon ilikataa kumruhusu kuitumikia Togo katika
Kombe la Mataifa ya Afrika litakaloanza Januari.
Lakini ripoti kutoka
Ufaransa zinasema uhamisho huo umeshindikana kwa sababu mahitaji ya straika huyo
aliyoyatoa katika mkutano huo.
Inadaiwa Adebayor
alitaka ndege aina ya helikopta kwa ajili ya kumpeleka mazoezini, akodishiwe
mpishi maalumu na nyumba ya kifahari yenye bwawa la kuogelea.
Kocha wa Lyon
alikaririwa akisema: “Tuna sehemu maalumu kwa ajili ya kuishi kikosi chetu na Manu,
niliandaa kukutana naye kwa ajili ya kunywa kahawa jijini Lyon.
... kwa hili naomba niombwe radhi.
“Lakini, kwa mshtuko,
wakati alipowasili aliagiza whisky badala ya kahawa. Pia alikuwa na sigara ikining’inia
mdomoni mwake.”
Hata hivyo, Adebayor ambaye
ni mchezaji wa zamani wa Arsenal na Manchester City amekanusha madai hayo kabla
ya kutaka kuombwa radhi.
Katika waraka wake wa
Alhamisi, Adebayor alisema: “Kwa kawaida huwa sitii neno kwenye majadiliano ya
uhamisho au tetesi za usajili lakini safari hii baadhi ya mambo yanatakiwa
kuwekwa sawa.”
“Lyon ilitaka
kunisajili na ikatoa ofa ya ndege kutoka Togo hadi Lyon kwa ajili ya kunisajili
kabla ya mchezo wao dhidi ya Marseille.
“Mkataba ulikuwa
umekubaliwa pande zote mbili na nilikuwa nisafiri kwa ajili ya kufanya vipimo na
kusaini fomu.
“Kwa bahati mbaya
sikuweza kwenda kwa wakati na wakamsajili straika mwingine kijana badala yangu.
Waliendelea kuniulizia kama ninaweza kwenda kuzungumza na kocha na mkurugenzi
wao wa soka kwa ajili ya kuangalia
uwezekano wa kutusajili wote.
...akiitumikia timu yake ya taifa ya Togo.
“Tulifanya mkutano Lyon
lakini kocha akaona haitakuwa sawa kutusajili wote kutokana na maendeleo ya
soka la vijana.
“Kwa madhumuni ya
kuondoa mashaka nilikunywa maji tu katika mkutano huo na sikuagiza whisky au
kuwa na sigara.”
Post a Comment