0


MANCHESTER, ENGLAND
BABA MZAZI wa Yaya Toure amemuomba Kocha, Pep Guardiola (pichani juu) kumpa nafasi kiungo huyo Muaivoricost kuitumikia Manchester City msimu huu.
Toure amewekwa pembeni uwanjani Eithad baada ya wakala wake, Dimitri Seluk kuingia katika malumbano na Guardiola.
Kiungo huyo wa City ameitumikia timu hiyo mara moja tu chini ya Guardiola katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa marudiano dhidi ya  Steaua Bucharest.

                          Pep akitoa maelekezo kwa Yaya.
Katika mchezo wa kwanza City ilishinda mabao 5-0 tangu hapo Toure hajacheza tena.
Baba wa Toure, Mory amelisema: “Nina wasiwasi kuhusu yeye. Ni tatatizo. Tunamuomba Guardiola kurudi chini. 
“Yeye ndiye bosi. Ninamuomba msamaha, amwache mtoto wangu afanye kazi yake.” 
Kiungo mwenye umri wa miaka 33- amebakisha mwaka mmoja tu katika mkatab wake klabuni hapo na mapema wiki hii Guardiola alisema hatampanga katika kikosi chake hadi atakapoombwa radhi na wakala Seluk kutokana na maneno yake kwenye vyombo vya habari.

Yaya.
Hata hivyo, Seluk alikataa kuomba radhi baada ya kudai kwam ba Guardiola anamdhalilisha Toure kwa kumuacha katika kikosi cha City kitakachoshiriki Ligi ya Mabingwa na kuendeleza vita ya maneno.

Yaya Toure akiwa kazini.
Baba wa Toure aliongeza: 'Yaya anaipenda klabu hiyo sana, ni mchezaji mzuri katika timu. Ana ari ya kucheza.
“Siwezi kuzungumza kwa niaba yake. Nadhani atabaki. Yeye ni mjanja. Atafanya uchaguzi mzuri baaaye.”
Hata hivyo, City imeanza msimu mpya vizuri bila ya uwepo wa Toure na iko kileleni katika Premier League ikiwa na wastani wa pointi 15.



Post a Comment

 
Top