0


MANCHESTER, ENGLAND
ROY KEANE amemchokoza Kocha Jose Mourinho kwa kumshushia kombora kufuatia kipigo cha mabao 2-1 cha Manchester derby Jumamosi iliyopita.
Kiungo huyo mkongwe wa Manchester United ameliondoa jina la ‘The Special One’ kwa Mourinho na kumpachika Pep Guardiola.

Mourinho
Akizungumza kwenye runinga baada ya Man City kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Borussia Moenchengladbach, Keane amempongeza kocha huyo Mhispania kwa kuwa na ushawishi wa haraka uwanjani Etihad.
Keane alisema anampongeza Guardiola kwa kuchukua maamuzi mazito katika klabu kama ya kuachana na kipa Joe Hart na kiungo, Yaya Toure na kuweka wazi kwamba hawamo katika mipango yake na akalisimamia jambo hilo kuhakikisha linatimia.
"Alisema ni kocha anayekubali changamoto – haogopi fujo zitakazotokea,” aliongeza.

Keane
"Sitapenda kugombana naye. Makocha wawili jijini Manchester. Mourinho anajiona yeye ni Special One, kwangu mimi huyo jamaa (Guardila) ndiye anayestahili."
Siyo habari zote nzuri kwa Guardiola ambaye timu yake ina rekodi nzuri katika Ligi Kuu ikiwa imeshinda michezo minne mpaka sasa pamoja na kwamba haibebwi na historia hiyo. “Lakini kila kitu kinaweza kubadilika,” alisema Keane.
"Tumeiona City ikianza vizuri kabla na baadaye ikapotea, lakini sidhani kama hilo linaweza kutokea chini ya mtu huyu (Guardiola)."
Maoni ya Keane yamekuja baada ya mmoja kati ya watu wanaaminika kuwa ni nembo ya Manchester United, Sir Alex Ferguson kumkumbatia bosi huyo wa City baada ya kupata ushindi Old Trafford.

Post a Comment

 
Top