MANCHESTER,
ENGLAND
JOSE MOURINHO amefunguka kwamba
haikuwa kazi rahisi kumshawishi kiungo, Paul Pogba kujiunga na Manchester
United.United ilimsajili Pogba kutoka Juventus na kuweka rekodi ya usajili wa dunia wa Pauni 89.3 katika dili hilo lililokamilika dirisha la majira ya joto.
Lakini bosi huyo wa zamani wa Chelsea, alisema haikuwa kazi rahisi kumfanya kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa kutua Old Trafford.
Pogba
"Oh, ilikuwa ngumu kumsahawishi.
Nilifanya naye mazungumzo mara nyingi sana kwenye simu, meseji za kutosha,"
alisema kocha huyo."Nadhani alikuwa akipata (simu) moja asubuhi kutoka kwa kocha wa klabu nyingine kubwa na nyingine mchana kutoka kwangu. Nilijaribu kumshawishi kuchagua upande wetu badala ya mwingine."
Hata hivyo, Pogba alipondwa kwa kiwango chake cha wikiendi kilichoshuhudia timu hiyo ikifungwa mabao 2-1 nyumbani na na wapinzani wao, Manchester City.
Kiungo wa zamani wa England, Jermaine Jenas, ambaye sasa ni mtangazaji alisema anaamini Pogba alihitaji kucheza kwenye mfumo wa 4-3-3 kuliko 4-2-3-1 ambao umekuwa ukitimiwa na United.
Mourinho
"Bado kuna wigo mpana katika Namba
10 kwa baadhi ya michezo, dhidi ya timu dhaifu labda, lakini kwa ujumla mfumo
wa 4-3-3 ndio ambao Pogba na Zlatan (Ibrahimovic) wanaweza kustawi.”"Pogba ni mchezaji mbunifu. Siyo mkabaji au unayepaswa kumpangwa kiungo cha chini kwa sababu, haijalishi uko vizuri kiasi katika majukumu hayo, huwezi kuwa na thamani ya Pauni 90 milioni."
Post a Comment