MADRID,
HISPANIA
DIEGO
SIMEONE (pichani) anaonekana kujipanga kuondoka Atletico
Madrid mwishoni mwa msimu ujao lakini klabu za Ligi Kuu England zitashindwa
kumnasa.
Inadaiwa
kwamba kocha huyo Muargentina mwenye mafanikio makubwa amejipanga kutua Italia.
Baadhi ya
vyombo vya habari vya Hipsania vimeripoti Alhamisi kwamba, Simeone amechukua uamuzi wa ajabu wa kupunguza mkataba wake kwa
miaka miwili na sasa atakuwa huru mwaka 2018 badala ya aliokuwa amejifunga
awali hadi 2020.
Mabadiliko
hayo yana nia ya kuhitimisha kile kilichomfanya kukaa katika klabu hiyo kwa
miaka saba.
Kocha Simeone
ndiye aliyedumu kwa muda mrefu Hispania na ameshinda mtaji matano akiwa na Atletico
na ameipeleka timu hiyo katika fainali mbili za Kombe la Ulaya na ameweka alama
yake kwenye historia ya klabu hiyo kama mmoja wa makocha wakubwa.
Kocha
Simeone ambaye pia ni nahodha wa zamani wa klabu hiyo na mshindi mara mbili haondoki
vibaya na anafahamu anaondoka mwaka 2018 itafanya kuiona klabu hiyo ikitumia
uwanja wake mpya wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 67,000 msimu ujao.
Pia, Kocha
Simeone ataondoka akiwa amepitia kipindi kigumu cha miezi 18 bila ya kuruhusiwa
kusajili mchezaji mpya baada ya rufaa ya klabu hiyo dhidi ya Fifa kutupiliwa
mbali.
Kocha huyo
mwenye umri wa miaka 46- nahodha wa zamani wa Argentina alisaini dili la
kuionoa Atletico Madrid Machi 2015 hadi 2020 lakini alikiri baada ya fainali ya
Ligi ya Mabingwa msimu uliopita kwamba ataangalia mustakabali wake.
Na chanzo cha
ndani ya klabu hiyo kimesema kwamba, Atletico imefanya kazi kubwa kumbakisha
katika majira ya msimu wa joto.
Klabu mbili
za Paris Saint Germain na Inter Milan zimekuwa zikivutiwa na huduma yake lakini
hakuna kati yao walioweza kumnasa. Simeone alikwa akisita kuhamia PSG na
mkatana wake mrefu lilikuwa likimaanisha
fidia kubwa iliyoiweka mbali Inter.
Mchezaji huyo wa zamani wa Ligi ya Italia ya Serie A, ameipa
nafasi Italia kama sehemu yake atakayotua na Inter inaweza kumpata bure, baada
ya kupunguza mkataba wake kama itaweza kusubiri hadi 2018.
Post a Comment