0


MANCHESTER, ENGLAND
MANCHESTER CITY imeifunga Manchester United mabao 2-1 na kujiweka katika nafasi nzuri kuanza msimu wa Premier League uwanjani Old Trafford.
City, langoni ilimweka kipa, Claudio Bravo na kumwanzisha Kelechi Iheanacho kuchukua nafasi ya Sergio Aguero aliyefungiwa, ilitawala mchezo mapema na United ikionekana  kuusoma mchezo.

Vijana wa Pep Guardiola walipata  bao la kuongoza katika dakika 15. Mpira mrefu kutoka kwa beki wa kushoto Aleksandar Kolarov ulipigwa kichwa na Iheanacho na kuwekwa katika njia ya Kevin De Bruyne, aliyetumia kusita kwa beki Daley Blind kuukwamisha wavuni.

Kutoka hapo, City iliendelea kutawala mchezo na United ambayo ilianza na Henrikh Mkhitaryan na Jesse Lingard katika nafasi za Juan Mata na Anthony Martial, hawakuza kumudu ari waliyokuwa nayo wapinzani wao.
Ujanja wa De Bruyne wa kukimbia na kuitumia mipira ya kati upande wa City dhidi ya wapinzani wake, ulimsaidia mchezaji huyo wa kimataifa wa ubelgiji kutengeneza bao la pili kwa City baada ya dakika 35.

Aligeuka katika nafasi ndani ya boksi akapiga krosi kuliangalia lango na akapiga ndani ya posti. Iheanacho, aliyekuwa akicheza na Blind, alipiga mpira uliorudi na na kuifungia City bao la pili.
Lakini mchezo wa kujihami wa City kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika uliipa United matumaini.

Kipa Bravo alichanganyana na  beki wake, John Stones kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Wayne Rooney na Zlatan Ibrahimovic kwa uhakika akaukwamisha wavuni na kumfanya kufunga bao la nne katika michezo minne.

Katika dakika za nyongeza, United ilionekana kujiamini kuwa ingeweza kusawazisha kufuatia krosi ya Rooney ilimkuta Ibrahimovic akiwa peke yake  lakini mpira wake a kichwa uliokolewa na kipa Bravo.

Mourinho alifanya mabadiliko mawili kwa kuwatoa Mkhitaryan na  Lingard na kuwaingiza Marcus Rashford na Ander Herrera.
Katika dakika ya 60, Rashford alimzunguka beki Bacary Sagna kabla ya kupiga krosi kwa Ibrahimovic aliyepaisha.

United ilijaribu kuwazuia City waliokuwa wakicheza mchezo wao wa pasi na kuutawala mchezo huo kama walivyokuwa wakifanya kipindi cha kwanza.

Kocha Guardiola alimtoa Iheanacho na nafasi yake ikachukuliwa na kiungo mkabaji Fernando, na kuicha City kucheza bila ya kuwa na mshambuliaji halisia.
Pamoja na jitihada za pande zote mbili, hakuna jitihada zilizozaa matunda na kumpa Guardiola haki ya kumtambia Mourinho katika mchezo wa kwanza wa Manchester derby.

Matokeo hayo yameifanya leaves City kuwa kileleni mwa Premier League ikiwa na pointi 12 baada ya michezo mine, pointi tatu mbele ya United.

Post a Comment

 
Top