0


MANCHESTER, ENGLAND
YAYA TOURE hataichezea Manchester City tena hadi Kocha Pep Guardiola atakaombwa radhi kutokana na maneno aliyoyatoa wakala wake, Dimitri Seluk.
Bosi huyo hajapendezwa na kauli ya Seluk ambaye ndiye mshauri mkubwa wa Toure, aliyesema  kitendo cha Guardiola kumweka benchi kiungo huyo ni cha kumdhalilisha mchezaji huyo mkubwa.

Guardiola
"Ilikuwa ni vigumu kwangu kumuacha (Toure) katika Ligi ya Mabingwa- vigumu sana," Guardiola alisema kwenye mkutano Jumanne. "Namjua, ni mchezaji mzuri, lakini ilikuwa vigumu kwangu pia kumwacha Aleix Garcia, (wao) ni wachezaji wawili ambao nimewaacha, kwa sababu orodha ni orodha.

                                  ....akifunguka yamoyoni
"Lakini siku moja baadaye wakala wake alizungumza– wakati huo- Yaya nilishamuacha. Mpaka Seluk atakaporudi kwenye kwa waandishi wa habari, au kwa marafiki zake wa vyombo vya habari, ana ujasiri wa kunipigia simu, kitendo cha kwanza anachopaswa kufanya ni kuiomba radhi Manchester City.


....Toure, hatacheza kama Seluk hataomba radhi.
“Kitu cha pili kuwaomba radhi wachezaji na baadaye wakufunzi. Kama atafanya hivyo, Yaya atakuwa sehemu ya kundi na atakuwa na nafasi ya kucheza michezo yote.
“Nikiwa kama kocha, siwezi kukubali, kila wakala pindi mchezaji wake anapokuwa hachezi aende kwenye vyombo vya habari na kuzungumza na kuzungumza na kuzungumza. Inategemea."

Seluk anapaswa kuomba radhi.
Hata hivyo, Seluk aligoma kuomba radhi baada ya kukaririwa na Sky Sports akisema kwamba : "Naweza kusema chochote ninachotaka  na Guardiola hawezi kunizuia."
Kiungo Toure amecheza mchezo mmoja tu City msimu huu- mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Steaua Bucharest- na hakushiriki katika kikosi cha City katika michezo miongine saba.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33- pia aliachwa katika kikosi cha Ligi ya Mabingwa cha Kocha Guardiola- sambamba na kinda wa Kihispania Aleix Garcia, ambaye amekaa benchi la City katika michezo miwili ya mwisho ya Premier League na alianza katika mechi ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Bournemouth wikiendi iliyopita.

Toure hatacheza dhidi ya Swansea.
Katika kupigilia msimu katika kidonda, Guardiola alisema Toure, ambaye amestaafu soka la kimataifa Jumanne, hatakuwamo katika mchezo wa Kombe la Ligi (EFL) Alhamisi dhidi ya Swansea City uwanjani Etihad.
"Najua jinsi Seluk anavyompenda Yaya Toure, kama ananipenda nami, aombe radhi kwa Manchester City kwa kile alichokizunzungumza kwa waandishi wa habari," alisema Guardiola.
"Siwezi kufikiria enzi zangu nilipokuwa mchezaji, wakala wangu aende kwenye vyombo vya habari na kuzungumza dhidi ya Johan Cruyff, kuhusu hili na lile.

Guardiola
"Labda ni zama mpya za sasa, kipindi cha mabadiliko, lakini mimi ni mtu wa zamani. Ni mtu wa kizazi cha zamani, na kocha wa kizazi cha zamani anapaswa kuwafanya wachezaji wafanye kazi zao na mkufunzi afanye kazi yake, na leo mawakala wanaamini ni wao zaidi ya walivyo.
"Kama ana tatizo angeweza kuwasiliana na Mkurugenzi wa Michezo, Txiki Begiristain au klabu na kufanya mazungumzo, hadi atapozungumza, Yaya hatacheza."
Toure alikosa mazoezi wiki ilioyopita kutokana na kuumwa kipanda uso lakini amerudi kujiunga na kikosi cha kwanza.
Lakini Guardiola hakumjali kufuatia kile kilichozungumzwa na Seluk mwezi Septemba.

        TUJIKUMBUSHE
Seluk alisema: "Kama City haitashinda Ligi ya Mabingwa nadhani Pep anapaswa kuomba radhi kwa kumnyanyasa mchezaji mkubwa kama Yaya."

Post a Comment

 
Top