0


MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO (pichani chini) ametoa sababu ya kufungwa kwa timu yake ya Manchester United Jumapili baada ya kuambulia kipigo cha tatu ndani ya siku nane.
Kocha huyo wa United amewatupia lawama wachezaji wake kwa kushindwa kujifunza  kutokana na makosa ya mchezo wa Manchester derby ambapo timu yake ilifugwa maboa 2-1.

Na akamtupia lawama beki wake wa kushoto, Luke Shaw kwa kushindawa kutimiza majukumu yake dhidi ya Camilo Zuniga.
“Nilijua nitakuwa na kazi,” alisema Mourinho, ambaye hajawahi kufungwa michezo mitatu mfululizo tangu alipokuwa kocha wa Porto mwaka 2002.

Mourinho akizungumza na Shaw.
“Lakini bao la kwanza la Man City na bao hili la (Watford) pili yanafanana, unaweza kuona kuna kufanana kwa ajabu.
“(Aleksandar) Kolarov alipata mpira katika mazingira magumu katika kona na wachezaji wangu badala ya kwenda kumkaba walimwachia nafasi. Leo katika bao la pili, (Nordin) Amrabat akiwa upande wa kulia, beki wetu wa kushoto (Shaw) alikuwa umbali wa mita 25, badala ya mita tano. Lakini pamoja na kuwa mita 25, unatakiwa kukimbia na kukaba. Lakini hapana, tumesuburi.
“Hii ni suala la ufundi lakini pia ni tabia ya akili ya mtu. Katika wiki kadhaa, kila kitu kama hiki kitakuwa sawa. Hii ni kazi yangu.”

Shaw akiwa umbali mita 25 na Nordin Amrabat.
Mourinho pia alipatwa na shaka na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake katika kipindi cha kwanza, alikiri kwamba alitegemea kiwango bora baada kufuatia vipigo vilivyofuatana vya Manchester City katika Ligi Kuu na  Feyenoord katika Europa League Alhamisi iliyopita.
“Ilikuwa ni mwanzo wa mchezo ambapo walipata nafasi nzuri za kufunga. Hilo linakatisha tamaa. Kulikuwa na kutokuelewana kati ya kipa David de Gea na beki Chris Smalling- wachezaji wawili wakubwa wenye uzoefu, kunakuwa hakuna mawasiliano.”

Mourinho pia alimtupia lawama mwamuzi wa mchezo huo, Michael Oliver, akilalamikia kuachia faulo aliyofanyiwa, Anthony Martial na kuifanya Watford kufunga bao la kuongoza lililopachikwa na Etienne Capoue.

Mourinho aliong eza: “Makosa ya mwamuzi na msaidizi wake hayako katika uwezo wangu. Siwezi kufanya chochote. Katika kipindi cha pili tulikuwa bora, tulisawazisha na baada ya hapo kipa wa Watford (Heurelho) Gomes aliokoa shambulizi na bahati ni jambo ambalo hatuwezi kulidhibiti.

Shaw akiwa ameachwa huku Zuniga akifunga bao la pili.


“Hatuwezi kumdhibiti mwamuzi, hatuwezi kudhibiti bahati.”
Mourinho alikumbushia kitendo cha mwamuzi kukataa penalti ya United dhidi ya City na bao la kuotea la Feyernoord.

Post a Comment

 
Top