MANCHESTER, ENGLAND
PAUL SCHOLES
ameibuka tena na safari hii amemkosoa kiungo aliyevunja rekodi ya uhamisho wa
dunia wa Manchester United, Paul Pogba.
Scholes
kiungo wa zamani wa timu hiyo amesema Pogba hachezi kama mchezaji ambaye United
imemnunua kwa Pauni 100 milioni.
Pogba
Baada ya
kung’ara katika mchezo wa kwanza dhidi ya Southampton uwanjani Old Trafford,
Pogba hajafanya vizuri katika michezo miwili, ule wa Ligi Kuu dhidi ya
Manchester City ambapo United ililala mabao 2-1 na wa hivi karibuni wa kipigo
cha bao1-0 dhidi ya Feyenoord katika Europa League.
“Ameonyesha
jitihada ndogo sana mpaka sasa,” alisema Scholes. “Usiku huu, tena, hakuwa na katika
kiwango bora. Nadhani atakuwa vizuri. Bado ni mapema sana.
“Kuna wakati
sikuwa nafahamu anacheza katika nafasi gani. Amefiti kwenye nafasi anayocheza? Ameambiwa acheze anapotaka?
Scholes mwenye kipaza sauti.
“Anajaribu
kuwapo kila sehemu kwa wakati mmoja. Nadhani
anajaribu kufanya mambo mengi akiwa na mpira.
“Anajaribu
kuwapita wachezaji watatu, wanne. Anakimbia na mpira. Anawezan kufanya kazi
ikawa nyepesi zaidi.
“Huyo siyo
mchezaji ambaye Manchester United iliyomnunua. Hawakumnunua Lionel Messi ambaye
anapiga chenga wachezaji watano na kusimama kwenye kona muda wote.
“Wamemnunua
kiungo mwenye nguvu, imara ambaye anaweza kupora mipira. Ana akili, anaweza
kupeleka mipira mbele, anaweza kukimbia.”
Pogba dhidi ya Man City
Lakini Scholes
hana wasiwasi na uwezo wa kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa
miaka 23.
“Kama
anaweza kucheza mara moja na kuachia, kupeleka mipira kwa Zlatan (Ibrahimovic) na
kukimbia, hakuna atakayemuweza,” alisema. “ Ana kasi na nguvu sana.”
Pamoja na
kusajili wachezaji wanne katika dirisha la majira ya joto, Scholes anaamini
klabu yake hiyo ya zamani inambidi kurudi sokoni kumaliza tatizo la Pogba.
Scholes alisema
Mfaransa huyo anateseka kwa sababu ya kukosekana kwa mchezaji mbunifu na mwenye
nguvu katika kikosi cha United.
Modric
Kiungo huyo mchezeshaji
mwenye mfano wa Andrea Pirlo- Muitaliano mwenye kipaji aliyekuwa akiendesha
mambo na kuwa injini ya Juventus enzi Pogba akiwa na vigogo hao wa Turin.
“Anahitaji
kuwa sambamba na kiungo mwenye kontroo,” alisema Scholes.
“(United) wanahitajika
kwenda sokoni kwa ajili ya kumnunua mtu kama huyo. Michael (Carrick) anao uwezo
huo.
“Lakini bado
anahitaji kiungo huyo mwenye uwezo wa kumiliki, anayeweza kumlinda kila Paul
anapokwenda na kumiliki mchezo wa soka.
Kroos
“Najua (Mourinho)
ana furaha na wachezaji wanne aliowanunua lakini bado anahitaji aina hiyo ya
mchezaji. Luka Modric au Toni Kroos (viungo wa Real Madrid) wanafaa.
“Nadhani
hawa wachezaji wanapatikana. Nadhani Pogba atakuwa bora zaidi akicheza na aina
hiyo ya wachezaji.”
Post a Comment