BARCELONA,
HISPANIA
NEYMAR (pichani) amethibitisha kufanya
mazungumzo na Mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain katika dirisha la
usajili la majira ya joto kabla ya kukubali dili la mkaba wa miaka mitano na Barcelona.Wakala Wagner Ribeiro aliweka wazi mapema wiki hii kwamba Neymar alifanya mikutano miwili na mabingwa wa Ufaransa- mmoja ukiwa Kisiwa cha Ibiza na mwingine jijini Sao Paulo-na straika huyo wa Brazil hakukana madai hayo.
Kwa kweli, fowadi huyo mwenye umri wa miaka 24-alisema kwamba alikuwa na majadiliano na klabu mbalimbali, lakini aliongeza hamu yake ilikuwa kuendelea kubaki Barca.
"Ndio, tulifanya majadiliano na watu wengi, siyo mtu mmoja (na PSG)," alisema katika mkutano wa waandishi wa habari Alhamisi.
"Lakini niliamua kubaki Barca kwa sababu najihisi niko nyumbani hapa. Nina furaha na wachezaji wenzangu na mimi ni mtu wa Barca."
Ribeiro alisema kwamba Neymar angeweza kupata Euro 40 milioni kwa mwaka jijini Paris kwa mwaka baada ya kukatwa kodi, na ndege binafsi ambayo angeitumia kwenda nayo Brazil kwa ajili ya michezo ya timu ya taifa na shea katika mlolongo wa hoteli zikiwa kwa jina lake kama sehemu ya ofa ya kutua PSG.
Hata hivyo, pamoja na kukiri mazungumzo hayo,Neymar hakutaka kuingia kwa undani na kufafanua kile kilichowekwa juu ya meza kama angekuamua kuachana na Barca.
"Siwezi kuthibitisha dau lilitajwa na Wagner (Ribeiro) kwa sababu sipendi kuzunguzmzia kuhusu namba," alisema.
"Kama nilivyosema nilikuwa na mazungumzo na timu nyingi, (PSG) haikuwa peke yake. Lakini niliamua kubaki hapa; nina furaha hapa."
Dili jipya la Neymar limemfunga katika klabu hiyo ya Catalunya hadi mwaka 2021 na hafikirii kama ataondoka Camp Nou kwa sasa, pamoja na kuendelea kwa tetesi kuhusu maisha yake ya baadaye.
Wagner Ribeiro
"Sitazamii kujiona nikiwa nje
ya Barcelona," aliongeza. "Ni kitu ambacho siwezi kukifikiria kwa
sababu ninajihisi niko nyumbani. Najisikia furaha hapa."Ninajiona muhimu, kama mtu mwingine katika timu, na ninadhani kwamba hilo linaweza kuisaidia timu. Nadhani utakuwa msimu mzuri kwangu na kwa timu."
Mbali na PSG, klabu za Manchester United na Real Madrid zilitajwa kuwa na nia ya kumtwaa Neymar kabla hajatiwa kitanzi katika mkataba mpya na Barca.
Post a Comment