LONDON, ENGLAND
ARSENAL ina uhakika wa kufanya
makubaliano ya dili jipya na kiungo, Mesut Ozil lakini iko katika wasiwasi mkubwa
juu ya straika wake, Alexis Sanchez kama atasaini mkataba mpya, chanzo ndani ya
klabu hiyo kimefichua.The Gunners wamekuwa na mazungumzo ya kutaka kuingia mikataba ya muda mrefu na wachezaji hao wawili kwa miezi kadhaa sasa, na mikataba yao ya sasa inaisha mwaka 2018.
Chanzo ndani ya klabu hiyo kimesema kwamba, majadilino ya Ozil kubaki Kaskazini mwa London yanaendelea vizuri. Hata hivyo, kumekuwa na wasiwasi juu ya Sanchez, anayedai kutaka kiingizwe kifungu cha kuuzwa katika mkataba wake na vilevile kuongezewa mshahara wake hadi kufikia Pauni 35 milioni kwa wiki.
Kwa
mujibu wa mkataba wake wa sasa, Sanchez analipwa Pauni 140 milioni kwa wiki,
akiwa kwenye kundi la mastaa wachache wanaolipwa fedha nyingi uwanjani Emirates.
Mabingwa wa Italia, Juventus mara
kadhaa wamehusishwa kuondoka kwa Sanchez katika usajili wa dirisha la majira ya
joto na bado wanaendelea kufuatilia kile kinachoendelea Emirates.Straika huyo wa kimataifa wa Chile alitua Arsenal akitokea Barcelona kwa dau linalodaiwa kufikia Pauni 35 milioni mwaka 2014, wakati kiungo wa kimataifa wa Ujerumani, Ozil alijiunga na klabu hiyo kwa dau lililovunja rekodi ya usajili wa klabu Pauni 42.5 milioni akitokea Real Madrid mwaka 2013.
Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger hivi karibuni aliweka wazi kwamba majadiliano yameanzishwa na klabu yake ili kuweza kujua hatma za wachezaji hao.
Post a Comment