LIVERPOOL,
ENGLAND
DANNY
MURPHY amefichua kwamba ilikuwa bado nusu tu Jose
Mourinho (pichani juu) awe kocha wa Liverpool.
Murphy ambaye alikuwa
kiungo wa zamani wa Liverpool alisema Mourinho aliitaka sana kazi hiyo na alikosa raha alipoikosa.
... Mourinho akiwa na Benitez
Kiungo huyo
alidai bosi huyo wa sasa wa Manchester
United na Rafa Benitez walikuwa washindani wawili waliowania nafasi hiyo mwaka 2004,
lakini mabosi wa Liverpool walimchagua Benitez kwa sababu alikuwa na mafanikio
Hispania.
Kocha Mourinho,
ambaye alikuwa akiinoa Porto wakati huo, alijiunga na Chelsea mwaka huohuo.
Murphy alifunguka: “Wakati
Benitez alipochaguliwa kuwa kocha wa Liverpool, ilikuwa ni kati yake na Mourinho.
Nalijua hilo kwa uthibitisho. Mourinho aliitaka sana kazi ya kuinoa Liverpool.
Kocha wa sasa wa Liverpool, Jurgen Klopp akiwa na Mourinho.
“Lakini Liverpool ilimchagua
Benitez, kwa sababu alikuwa ametoka kushinda
taji la Ligi ya Hispania na Kombe la UEFA akiwa na Valencia na walidhani
alikuwa bora kuliko mtu mwingine ambaye alikuwa ameshinda taji mara moja, na
wakati huo, in Ureno.
“Najua Mourinho aliumia
sana kuikosa nafasi hiyo ambayo alikuwa akiitaka sana."
Murphy aliichezea Liverpool kati
ya mwaka 1997 na 2004 lakini alitimuliwa
muda mfupi baada ya kuwasili kwa Benitez.Alijiunga na Charlton kabla ya kwenda kuzitumikia Spurs, Fulham na Blackburn.
Murphy akinyanyua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mkongwe huyo alifanya utani
aliposema, siyo Mourinho tu aliyechanganyikiwa.Alisema: “Hata mimi pia, kwa sababu Benitez alipokuja alinikataa. Nilichanganyikiwa pia, hakuwa Mourinho peke yake kwa sababu Benitez hakutaka nibaki!”
Post a Comment