0


MANCHESTER, ENGLAND
ARSENAL na Manchester City zimevutiwa na huduma za Muivory Coast, Yaya Toure, lakini wakala wake, Dimitri Seluk ametia neon.
Wakala Seluk amesema timu hizo zimeonyesha nia ya kumtaka kiungo huyo.
Toure mwenye umri wa miaka 33, anaonekana kutohitajika Manchester City chini ya Kocha Pep Guardiola  na ameachwa katika kikosi cha wachezaji 21-watakaoshiriki Ligi ya Mabingwa.

Wakala Seluk amesisitiza kwamba haiwezekani kwa kiungo huyo kujiunga na United au Arsenal,  na akaweka wazi kwamba kiungo huyo ana ofa kutoka China, Uturuki, Italia na Marekani,  na ataangaliab uwezekano wa kusaini makubaliano ya mkataba wa awali  na klabu nyingine Januari.
Kiungo Yaya Toure yuko kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake Etihad, ambako ameshinda  mataji mawili ya Premier League baada ya miaka yake sita aliyojiunga akitokea Barcelona.
"Yaya Januari anaweza kusaini makubaliano ya awali ya mkataba na klabu ya nje ya England," Seluk alisema. 
"Tunatarajia atakuwa na ofa nyingi kutoka klabu mbalimbali. China na Marekani bila shaka wanamhitaji  lakini tunatarajia ofa nyingine kutoka England na Ulaya.
"Yuko katika kiwango kizuri, afya nzuri, nadhani amepungua kwa kila saba.
"Labda hilo linaweza kuwa  jambo zuri kwa Guardiola, lakini hata hivyo, Zlatan Ibrahimovic hakufaa wakati walipokuwa Barcelona.”

Seluk na Yaya Toure
Yaya Toure ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mara nne, na Seluk pia anaamini Waafrika wengi wataisapoti Manchester United katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Manchester City, kufuatia kile ambacho City inamfanyia mteja wake.
"Watapoteza mashabiki mamilioni  kutoka Afrika kwa sababu ya uamuzi wa Guardiola," Seluk alisema.
"Sasa watashabikia Manchester United. Watu wengi wa Afrika  wanasema hawataangalia tena mechi za City katika TV."

Post a Comment

 
Top