MANCHESTER,
ENGLAND
ZLATAN
IBRAMOVIC amempandisha presha kipa wa
Manchester City, Claudio Bravo kabla ya mechi ya Manchester derby Jumamosi.
Straika
Ibrahimovic anatarajia kuongoza safu ya ushambuliaji ya Manchester United
katika mechi hiyo ya mahasimu itakayopigwa Old Trafford ambapo Jose Mourinho na
Pep Guardiola watakutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu
England.
Wakati
dunia nzima ikisubiri mechi hiyo, Ibrahimovic ameanza kumchokoza Bravo, ambaye
inaaminika atakuwa golini kwenye mechi hiyo.
Fowadi
huyo mwenye umri wa miaka 34 alituma video kwenye ukurasa wake mtandao wa
kijamii akionekana akimtumia vifaa vya mazoezi kipa Bravo kwa sababu atakuwa
anavihitaji kabla ya kumkabili Jumamosi.
Kisha
Ibra aliandika ujumbe huu: “Karibu Manchester! Vifaa vya mazoezi hivyo hapo,
najua utavihitaji sana. Tuonane Jumamosi.”
Kipa wa Man United, Bravo.
Ibrahimovic
tayari ameshafunga mabao matatu katika Ligi Kuu England msimu huu na sasa
anasubiri kuonyesha makali yake dhidi ya kipa Bravo kwenye mechi hiyo ya
Manchester derby.
Post a Comment