LONDON, ENGLAND
EDDIE
HOWE ndiye kocha anayepewa nafasi kubwa ya kuubeba msalaba wa Arsenal Wenger
ndani ya Emirates.
Kocha
huyo Mwingereza kwa sasa anakionoa kikosi cha Bournemouth na ndiye anayejadiliwa
sana kwenye korido za Emirates kuwa anafaa kurithi mikoba ya Mfaransa, Arsene
Wenger wakati atakapong'atuka ukocha na kupandishwa nafasi za juu klabuni hapo.
Kocha Wenger akiwa na Howe.
Howe
anawavutia wengi kwenye klabu hiyo ya ikiwamo wafanya maamuzi katika klabu hiyo
ya Ligi Kuu England. Howe aliisaidia
Bournemouth isishuke daraja msimu uliyopita, anafuatiliwa sana na Arsenal inavutiwa
kwa namna anavyofanya mambo yake uwanjani.
Mkataba
wa Wenger unafika tamati mwishoni mwa msimu huu na hakuna mazungumzo ya
kuongeza mwingine, licha ya kwamba Mfaransa huyo aliambiwa na mmoja wa wamiliki
wa klabu hiyo, Stan Kroenke kwamba anaweza kuendelea kubaki klabu hayo, huku
wakiamini Howe anaweza kuingoza timu hiyo kama Wenger ataamua kung'atuka.
Howe
Wenger
ambaye analipwa Pauni 7.5 milioni kwa mwaka ameambiwa kwamba ana kibarua cha
maisha yake yote klabuni hapo akitengenezewa nafasi ya kuwa mkurugenzi wa
ufundi pindi kocha mpya atakapopatikana.
Wenger, amempeleka kwa mkopo kiungo Jack
Wilshere kwenda Bournemouth hiyo inatokana na kupendezwa na utendaji wa Kocha Howe.
Post a Comment