0


LIVERPOOL, ENGLAND
JURGEN KLOPP anaumiza kichwa na kishindwa kuamua kipa yupi ampange langoni wikiendi hii kati ya Loris Karius na Simon Mignolet wakati timu hiyo itakapokabiliana na Hull City.
Kipa Karius alisajiliwa kwa Pauni 4.7 milioni kutoka Mainz ya Ujerumani katika dirisha la majira ya joto, ili kumpa changamoto Mignolet alicheza michezo ya maandalizi kabla ya  kuvunjika mkono, alipangwa kuchukua namba katika Premier League ili kumpa changamoto Mignolet kupigania namba.

Mignolet akimpongeza Karius.
Hata hivyo, baada ya kuwekwa benchi michezo miwili ya ligi alionyesha upinzani katika mchezo wa ushindi wa Kombe la Ligi (EFL) dhidi ya Derby.
Hata  hivyo, Kocha Klopp hajajifunza zaidi kwa kipa huyo Mjerumani, ambaye amekuwa akitawala mipaka ya nje ya eneo lake la hatari, katika mchezo wa ushindi wa mabao 3-0  kutokana na kazi ndogo aliyoifanya katika mchezo huo   kwani aliokoa hatari moja dhidi ya straika, Darren Bent na kucheza krosi moja tu kati ya mbili.

Karius bado hajapata changamoto za kutosha.
Kipa Mignolet amekuwa akiitumikia timu hiyo ndani ya miaka miatatu uwanjani Anfield lakini kiwango chake hakikuwa cha kuridhisha, na kutoa nafasi ya kuletewa mpinzani wa kumpa changamoto.

“Siyo suala la kutangaza kikosi  lakini tunapaswa kufikiria kwa njia sahihi,” alisema Klopp.
“Sijawahi kuwa kipa – baba yangu alikuwa kipa kwa hiyo nina uzoefu kidogo katika nafasi hiyo- lakini kwa kiasi fulani ni tofauti na wachezaji wa ndani ambao hakuna anayeweza kuuliza kama anaanza na mwingine akaanza wakati mwingine.

Mignolet akiwa benchi dhidi ya Derby.
“Sina uhakika, nitafanya uamuzi wa mwisho kwa ajili ya mchezo unaofuata lakini hamiaanishi tutaendelea hivyo kwa miaka mitano ijayo.
“Ni uamuzi wa kiwango cha juu  kwa sababu ninafurahishwa na wote wawili lakini hakuna ninaloweza kusema zaidi kuhusu hilo hapa.
“Kama ninavyofanya kila siku kwa ajili ya mchezo unaofuata ni uamuzi wa kwa ajili ya mchezaji na siyo dhidi ya mchezaji mwingine – mnapaswa kusubiri na mtaona.”
Mchezaji mwingine ambaye pia anapaswa kusubiri na kuona kama atajumuishwa kwenye kikosi cha  Jumamosi ni Daniel Sturridge, ambaye alikosa mchezo wa ushindi dhidi ya Derby baada ya kutofanya mazoezi.

Karius akiokoa hatari mbele ya Bent.
“Daniel amefanya kitu fulani kama jaribia la mwisho jana, kwa hiyo ana siku tatu bila ya kufanya mazoezi  lakini anatakwia kufanya mazoezi leo,” alisema Klopp.
“ Kuna masuala kadhaa baada ya mchezo (wa Chelsea Ijumaa). Kwa sasa tuna siku mbili nyingine hadi Jumamosi na tutaona nani amefanya mazoezi muda wote na yuko tayari kwa mchezo.

Kocha Klopp.
“Ni kwamba (kucheza kwa Sturridge) kutatokana na mazoezi. Adam (Lallana) na Gini (Wijnaldum) hawakucheza (dhidi ya Derby) lakini watakuwa tayari.” 

Post a Comment

 
Top