MADRID, HISPANIA
CRISTIANO RONALDO (pichani) amemshukia Xavi Hernandez baada ya kiungo huyo wa zamani wa Barcelona kudai
Ronaldo ana bahati mbaya kuzaliwa katika kipindi ambacho Lionel Messi amezaliwa.
Kiungo Xavi alimsifu
Mreno huyo kwamba ni mchezaji mzuri, lakini alisema ana bahati mbaya ya
kuzaliwa kipindi ambacho nyota wa Argentina amezaliwa.
Ronaldo akishangilia bao
Ronaldo alisaidia
timu yake kuifunga Osasuna mabao 5-2 akiwa ndio kwanza anarudi kutoka katika
majeraha.
Straika huyo
aliumia katika mchezo wa fainali ya Uero
2016 dhidi ya Ufaransa.
“Mchezaji anayetafutwa sana kwenye mtandao ni mimi,” alisema kwa hasira Ronaldo. “Wanaotaka kutokea kurasa za mbele (katika magazeti) au kutangaza vitu wanazungumzia kuhusu mimi.
“Mchezaji anayetafutwa sana kwenye mtandao ni mimi,” alisema kwa hasira Ronaldo. “Wanaotaka kutokea kurasa za mbele (katika magazeti) au kutangaza vitu wanazungumzia kuhusu mimi.
“Nitajari kitu gani
ambacho Xavi anasema? Anacheza wapi? Qatar au (sehemu nyingine), sijui. Ameshinda
kila kitu lakini kamwe hajashinda Ballon d'Or. Nimeshinda mara tatu.”
Straika Messi ameshinda
tuzo ya Ballon d'Or mara tano na anatazamwa kama mchezaji bora wa muda wote, lakini
Ronaldo anaamini anastahili tuzo hiyo.
Xavi
Akizungumza na Radio
ya Hispania mapema wiki hii, Xavi alisema: “Ni mjinga tu ambaye hawezi kutambua
kwamba Cristiano (Ronaldo) ni mchezaji bora. Lakini ana bahati mbaya kuzaliwa katika
zama sambamba na Leo (Messi).”
Jumamosi Ronaldo alifungia Madrid bao katika dakika ya sita uwanjani Santiago Bernabeu dhidi ya Osasuna na kuifanya kushinda katika mchezo wake watatu wa La Liga.
Jumamosi Ronaldo alifungia Madrid bao katika dakika ya sita uwanjani Santiago Bernabeu dhidi ya Osasuna na kuifanya kushinda katika mchezo wake watatu wa La Liga.
Messi
Mreno huyo alipondwa baada
ya kutoa maoni yake kuhusu Iceland katika michuano ya Euro 2016. Ronaldo alidai
wachezaji wa timu hiyo ya taifa wana fikra ndogo baada kushangilia sare dhidi
ya Ureno katika hatua ya makundi kama vile wametwaa taji.
Ronaldo pia alida
kama angekuwa Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, Real, angejipa dili kubwa
zaidi Madrid. Mkataba wake wa sasa unaisha mwishoni mwa 2018.
Xavi akiwa Qatar na klabu ya Al Sadd.
Staa huyo
aliongeza: “Kama ningekuwa Rais wa Real Madrid, ningejipa mwenyewe mkataba wa
miaka 10. Mpaka sasa sifikirii kuhusu kitu kingine kuhusu kazi yangu, kitu
ninachotaka ni kustaafu nikiwa Real Madrid. Hii ni klabu kubwa duniani na
inapaswa kuwa na wachezaji bora.”
Post a Comment