MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO ni kama vile amemfariji
nahodha wake, Wayne Rooney ambaye alikuwa benchi katika kikosi cha ushindi
kilichoichapa Leicester mabao 4-1 katika
mchezo wa Ligi Kuu.Kocha huyo Mreno amekataa kukubali kwamba mabadiliko ya kikosi chake, ikiwemo kumweka benchi Rooney, ndio sababu ya Manchester United kuikung’uta Leicester City uwanjani Old Trafford Jumamosi.
Rooney uwanjani
Bila ya Rooney na Marouane Fellaini,
United ilicharuka katika kipindi cha kwanza na kuongoza kwa mabao 4-0. Nahodha huyo wa United, ambaye amekuwa na mwanzo mbaya wa msimu huu, alikuwa kwenye benchi la timu hiyo kwa dakika zote 90.
Alipoulizwa kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30-, Mourinho alisema: " Bado ni mchezaji mkubwa kwangu, mchezaji mkubwa kwa United, na mchezaji mkubwa kwa nchi hii.
Rooney akiwa benchi.
"Ni mtu wangu, namwamini sana. Ana
furaha kwa wakati huu kama nilivyo miye na hii ni timu."Kocha huyo mwenye maneno mengi alipoulizwa katika mkutano wake na waandishi baada ya mchezo huo kama mabadiliko ndio sababu ya ushindi, Mourinho alijibu: "Hapana, sidhani. Nadhani matokeo hayo ni kwa sababu tulianza mchezo vizuri na hatukusimama mpaka mwisho. Kama timu inacheza vizuri, ni rahisi kuwa na uwezo binafsi.
Mourinho akiwahamasisha wachezaji.
"Nahodha wangu ni nahodha wangu.
Kama akiwa uwanjani au nyumbani, bado ni nahodha wangu, hilo siyo tatizo. “Katika mchezo wa leo dhidi ya timu kama Leicester, tulifikiria ufumbuzi kwetu ni kuwatumia vijana wawili wenye kasi na (Juan) Mata katika nafasi ambayo anaweza kuingiliana nao.
"Kama sijampanga (Marcus) Rashford, mnaniuliza kwa nini. Kama sijampanga (Jesse) Lingard, mnaniuliza kwa nini. Na siku zote mnapenda kuuliza kwa nini fulani hachezi.
Mchoro unaoonesha bao la Mata.
"Kuna wakati ninaposoma
mnachoandika, najihisi sijui kitu kuhusu soka. Kitu ninachokijua ni sheria za
mchezo. Ninaweza tu kuanza na wachezaji 11. Labda mtu aniambie sheria
imebadilika, naweza kuanza na wachezaji 11 tu."
Post a Comment