LONDON,
ENGLAND
ANTONIO
CONTE ana kazi kubwa. Bilionea na mmiliki wa timu hiyo, Roman Abramovich
aliitisha kikao cha benchi la ufundi alipofungwa na Liverpool.
Hali
inaweza kuwa mbaya zaidi baada ya kufungwa mabao 3-0 na Arsenal.
Kocha
Antonio Conte ameanza kujipanga upya ili kunusuru kibarua chake baada ya kikosi kukumbana na kichapo, tena dhidi ya
mahasimu wao wa jiji moja la London.
Kipigo
hicho kimezua mjadala na huenda Abramovich akaitisha kikao na bodi nzima.
Katika
kujinusuru, Kocha Conte sasa amefikiria kuwapiga chini mabeki wote waliocheza
mechi hiyo ya Arsenal na kuruhusu mabao ya kijinga.
Conte akishangazwa na kipigo.
Mabeki
Branislav Ivanovic na Gary Cahill walihusika kwenye bao la kwanza la Arsenal
kwa kufanya uzembe, lakini beki yao iliendelea kufanya makosa ambayo yameifanya
hadi sasa kuruhusu mabao 12 kwenye wavu wao.
Kitu
ambacho Conte anachosubiri ni mabeki wake wengine wa kati John Terry na Kurt
Zouma wapone na wakiwa fiti tu, moja kwa moja wanakuja kikosini na jambo hilo
litawagharimu waliocheza kizembe kwenye kipigo cha Arsenal.
Cahill akijutia.
Kocha
Conte anafikiria pia kumpiga chini beki wake mpya, Mbrazili, David Luiz kutoka
kwenye orodha ya mabeki wake wa kati chaguo la kwanza na ikifika Januari tu shughuli
ya kwanza itakayofanyika ni kuhakikisha anawanasa Leonardo Bonucci na Kalidou
Koulibaly.
Beki
mpya, Marcos Alonso ameonyesha kiwango kizuri kwa dakika chache alizocheza na
huenda panga hilo lisipite kwenye jina lake.
Mabeki wa Chelsea wakijiuliza.
Ukiwaweka
kando mabeki hao, Conte anawafikiria pia Michael Keane na Ben Gibson ambapo
amewatuma skauti wake kuhakikisha wanawafuatilia kwa karibu wachezaji hao ili
kuona kama wataweza kufiti kwenye kikosi chake ili kuondokana na shida ya
kuruhusu mabao ya kijinga.
"Unauliza
nilichukia kipindi cha kwanza? Jibu langu ni ndio, lakini huwa napenda kutozungumza
sana, kwa sababu ninafahamu kitu ambacho napaswa kukizungumza, nitazungumza na
wachezaji wangu kuwaeleza ukweli," alisema Conte.
Cahill
"Ni
kawaida. Kweli nilikasirika, lakini wachezaji wangu walikasirika pia. Hii ni
kwa sababu hatukufurahishwa na mchezo wetu na kiwango chetu. Sikulala, sikulala
kabisa."
Kwenye
orodha ya mabeki wa Chelsea waliopo kwenye kikosi hicho cha Mtaliano Conte ni
Cesar Azpilicueta, Cahill, Ivanovic, Terry, Luiz, Zouma, Ola Aina na Marcos
Alonso.
Cahill taabani.
Chelsea
kwa sasa inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na
pointi 10, pointi nane pungufu ya kuwafikia vinara Manchester City, ambao
wamekuwa na rekodi nzuri ya ushindi wa asilimia 100 tangu msimu huu uanze.
Nne
Bora ya Ligi Kuu England kwa sasa inaundwa na Man City, Tottenham Hotspur,
Arsenal na Liverpool, wakati vijana wa Jose Mourinho, Manchester United wakishika
nafasi ya sita, huku Everton ya Ronald Koeman ipo ikiwa nafasi ya tano.
Post a Comment